March 03, 2016

Roma Afungukia Uhusiano Wake na Dada’ke Kiba

SIKU chache baada ya kuzagaa picha zikimhusisha staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ na dada wa staa wa Bongo Fleva, Ali... thumbnail 1 summary
SIKU chache baada ya kuzagaa picha zikimhusisha staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ na dada wa staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba, Zabibu Kiba, Roma ameibuka na kutolea ufafanuzi kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi kama watu wanavyodhani na kwamba ni mshkaji tu.
Akichonga na Showbiz Xtra, Roma anayebamba na Ngoma ya Mtoto wa Kigogo alisema kuwa picha hizo alipiga kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wote studio.
“Sina uhusiano wa kimapenzi naye, Zabibu ni mshkaji wangu tu, siku hiyo alikuja akanikuta niko studio ndiyo nikapiga naye,” alisema Roma anayetarajiwa kufunga ndoa baada ya Pasaka na mpenzi wake wa siku nyingi, Nancy.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: