March 24, 2016

Paul Makonda hajalala, anaendelea kutafuta na leo kakutana na Balozi wa China…(+Video)

March 23 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alikutana na Balozi wa China nchini Tanzania na kujadiliana kuhusu namna ya kui... thumbnail 1 summary
March 23 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alikutana na Balozi wa China nchini Tanzania na kujadiliana kuhusu namna ya kuinua uchumi kwa vijana wa
Kitanzania na kusaidia elimu kwa wanafunzi.

‘Balozi wetu wa china amekuja kunitembelea katika ofisini yangu na kufahamu ninashughulika na nini kwahiyo tulizungumza vitu kadhaa ikiwemo changamoto mbalimbali ikiwemo ya wadogo zangu kukosa madawati Lakini pia nimemuelezea changamoto ya usafi kwamba mji wetu kwa sasa hivi upo kwenye kampeni ya usafiri’ –Paul Makonda

‘Ningependa kuona katika makampuni

yaliyopo tupate hata baadhi ya makampuni kutoka kwao pia yanayoweza kufanya usafi huo kwa maana kuchukua uchafu unaoonekana na kutengeneza mbolea na kuzalisha umeme’ – Paul Makonda
Itazame hapa video hii Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi baada ya kukutana na balozi wa China


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments