March 30, 2016

OBAMA: WANAHABARI NDIO WALIOMJENGA TRUMP.

Rais Barack Obama wa Marekani amelaumu vyombo vya habari kwa kukua kwa umaarufu wa mgombea wa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump. thumbnail 1 summary
Rais Barack Obama wa Marekani amelaumu vyombo vya habari kwa kukua kwa umaarufu wa mgombea wa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump.

Akihudubia hafla maalum kwaajili ya waandishi wa habari wa siasa bw Obama alisema sharti waandishi wa habari nao wawajibike kwani haitoshi tu ”kumpa mtu kinasa sauti ”

Bwenyenye huyo mbishi ambaye alijenga jina lake na kupata utajiri mkubwa kutokana na kuendesha na kumiliki migahawa katika maeneo mengi tu duniani anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican kuwania urais.

Trump, na wapinzani wake wanaowania tikiti ya chama chao cha Republicans wameratibiwa kukabiliana katika mdahalo wa runinga baadaye leo usiku.

Shirika la habari la CNN linaanda madahalo huo kabla ya kura za mchujo za jimbo la Wisconsin zinazoratibiwa kufanyika juma lijalo.


Japo hakumtaja Trump kwa jina ilikuwa bayana kuwa ndiye aliyelengwa na ujumbe wa Obama.

Anaposafiri ughaibuni, Obama anasema watu humuuliza nini kinachoendelea katika siasa za Marekani kwani’ sio mahali unakotarajia siasa zisizokuwa za kawaida”

Wanasiasa waandishi habari na umma kwa jumla wana wajibu wakati wa siasa kali kama hizi zinazoshuhudiwa kwa sasa Marekani.

Aliwashauri waandishi habari kupiga msasa habari wanazochapisha.


Haiwezekani kuwa mwanasiasa anaahidi vitu

ambavyo tunajua wazi kuwa hawezi kutimiza ilahali anaendelea kupeperushwa hewqani ,lazima nanyi mchukue jukumu la kuuliza maswali magumu na kutofautisha mbivu na mbichi.

Katika siku za hivi punde Trump alikashifiwa na wapinzani wake kwa kumgoa mkewe mpinzani wake ambaye ni gavana wa jimbo la Texas Ted Cruz.

Trump atakabiliana na mpinzani wake mkuu Ted Cruz katika uchaguzi wa jimbo la Wisconsin Aprili tarehe 5.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments