March 04, 2016

Arusha kupata njia nne kwa mara ya kwanza

Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli amezungumza na wananchi wa Arusha wakati wa uwek... thumbnail 1 summary
Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli amezungumza na wananchi wa Arusha wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya njia nne kwa mara ya kwanzaArusha.

Hafla ya uwekwaji wa jiwe la msingi lililowekwa na Rais Magufuli na Rais Uhuru Kenyatawa Kenya katika eneo la Tengeru Arusha ulihudhuriwa na viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Makamu wa Rais waBurundi Dk Joseph Butore.

Kwa upande wa Tanzania ujenzi huo utatekelezwa kwa awamu mbili, kwanza ujenzi wa njia nne kutoka Arusha hadi Tengeru yenye urefu wa Kilometa 14.1, ujenzi wa barabara ya mzunguuko “Bypass” yenye urefu wa Kilometa 42.4.

Wakati awamu ya pili ni ujenzi wa njia nne kuanzia Tengeru hadi Usa River yenye urefu wa Kilometa 8.2 na Usa River hadi Holili mpakani mwa Kenya na Tanzania yenye urefu wa Kilometa 100.2

“Nachoweza kusema ni kwamba nawashukuru kuja kwa wingi kushuhudia uwekwaji wa jiwe la msingi, kwa barabara inayotoka Arusha, Holili, Taveta na Voi yenye jumla ya Kilometa 234.3 ambayo inajengwa” >>> Rais Magufuli 

Unaweza kusikiliza hapa maneno ya Rais Magufuli


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: