January 10, 2016

Hii ndio habari ya Martial wa Man United inayoweza kuwagharimu wenye gazeti …

Gazeti la The Sun lilimuweka kwenye headlines mkali wa kucheka na nyavu wa Man United, baada ya kumuandika kuhusu stori za usaliti wa... thumbnail 1 summary


Gazeti la The Sun lilimuweka kwenye headlines mkali wa kucheka na nyavu wa Man United, baada ya kumuandika kuhusu stori za usaliti wa mapenzi. Mastaa wa soka huwa wanaingia kwenye headlines za usaliti wa mapenzi aliwahi kuingia katika headlines hizoJohn Terry wa Chelsea ila yeye kulikuwa na ushahidi sasa ni Anthony Martial wa Man United.


Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anatajwa kumsaliti mpenzi wakeSamantha, The Sun liemuandika Anthony Martial kumsaliti mkewe kwa mwanamitindo. Kitendo hicho cha The Sun kumuandika Martial ambaye mashabiki wa Man Unitedwanaamini ni mambo yake binafsi kinaweza kukigharimu chombo hicho kama Martialakiamua kukifungulia mashitaka.


Mambo kama hayo ya Martial hayakupaswa kuwekwa hadharani hata kama wanachosema kingekuwa kweli, na inatajwa kuwa watachukuliwa hatua kwa habari yao hiyo, ambayo inatajwa kuandikwa ili kuuza gazeti na inaonekana kama hakuna ushahidi.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: