October 06, 2015

Kumbe Marekani tatizo la watu kudownload muziki kinyume na Sheria bado ni kubwa sana tu!

Licha ya Marekani kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuwa na Sheria kali zinazodhibiti kudownload nyimbo kinyume na utaratibu uliowe... thumbnail 1 summary
Licha ya Marekani kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuwa na Sheria kali zinazodhibiti kudownload nyimbo kinyume na utaratibu uliowekwa, sources nyingi zinazotoa huduma ya kustream na kudownload muziki kama Tidal, Apple Music naSpotify za Marekani bado zinashindwa kudhibiti kwa asilimia mia moja vitendo vya watu kudownload nyimbo za wasanii kinyume na utaratibu na Sheria zilizowekwa! Tatizo ambalo hata kwa hapa kwetu Tanzania lipo sana.


Kwa mujibu wa utafiti mpya uliyofanyika na SeatSmart, soko la kudowload muziki kinyume cha Sheria Marekani halionyeshi dalili la kufa wala kupotea hivi karibuni… utafiti huo umeonesha kuwa muziki wa HipHop ndio unaoongoza kwa kuwa na downloads nyingi sana ambazo zipo kinyume na utaratibu wa kisheria!

Rapper Drake.

Wasanii kama Drake na Future kwa mwaka huu tu wametajwa kuwa wasanii wa HipHopambao ngoma zao ndio zinazoongoza kwa kuwa na downloads nyingi ambazo hazifuati utaratibu wala Sheria za jinsi ya kudownload nyimbo hizo… kwa mfano Album ya Future‘DS2’ iliotoka miezi michache iliyopita mwaka huu imeonekana kuwa na downloads nyingi ambazo sio halali kwa siku moja tu ikifuatiwa na ‘IYRTITL’ ya kwake Drake!

Rapper Future.

Muziki aina ya Pop, Rock, Country, na R&B nazo pia zimetajwa kuwa na idadi nyingi za downloads zilizopo kinyume na Sheria licha ya mipango mingi kuwekwa kudhibiti vitendo hivyo!

Nimefanikiwa pia kuzinasa baadhi ya picha za utafiti wa SeatSmart, zinazoonesha kwa kiasi gani download hizo zinafanyika na kuzisogeza kwako hapa chini…

Picha hii ya kwanza inaonyesha HipHop ndio inayoongoza kwa kuwa na downloads nyingi ikiwa na jumla ya idadi 456,270 za downloads zilizopo kinyume na Sheria.

Haya kwenye downloads za siku tu, Future na Drake ndio wasanii wanaoongoza kwa kuwa na nyimbo nyingi kwenye downloads zisizo halali!

Album ya Drake ‘If You’re Reading This, It’s Too Late’ inaongoza kwa kuwa na downloads nyingi kinyume na Sheria!

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: