October 28, 2015

INSTAGRAMU WAIFUNGIA AKAUNTI YA IDRIS SULTANI, SOMA HAPA KUJUA SABABU YA KUFUNGIWA

Instagram imeifungia akaunti ya mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan. thumbnail 1 summary

Instagram imeifungia akaunti ya mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan.

Idris ameimbia Bongo5 kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kuvunja masharti ya mtandao huo.

Amesema anadhani sababu za kufungikiwa kwa akaunti yake ni kutokana na kupost kipande cha video kutoka kwenye filamu ya The Interview iliyowahi kupigwa marafuku katika baadhi ya nchi.

“Nafikiria labda kutokana na ile part, ndio kitu pekee kilichosababisha kwasababu hakuna ukiukwaji mwingine wowote niliofanya,” amesema.

Idris amesema kitu pekee kinachoweza kusababisha mtu kufungiwa akaunti ya mtu bila taarifa ni pale anapoweka picha za utupu ama kama mtumiaji mwingine ametoa malalamiko kuhusu akaunti husika.

Anasema kwa sasa kila anapotaka kuingia kwenye akaunti hiyo anaambiwa ‘you account has been disabled.’

Hata hivyo amesema mchakato wa kuirejesha unaendelea na anaamini ndani ya wiki moja itakuwa imereja. Instagram wamewahi kuifungia akaunti ya Rihanna baada ya mrembo huyo kupost picha za utupu.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: