August 20, 2015

Ukame wa wana CCM Maguli kuhamia CHADEMA, Je Lowassa Amefilisika au Ameuziwa Mbuzi Kwenye Gunia?

Wakati Lowasa anahamia CHADEMA, alienda kwa tambo nyingi huku akiwaahidi viongozi wa CHADEMA kuwa kuna mafuriko ya wana CCM kuhama chama ... thumbnail 1 summary
Wakati Lowasa anahamia CHADEMA, alienda kwa tambo nyingi huku akiwaahidi viongozi wa CHADEMA kuwa kuna mafuriko ya wana CCM kuhama chama chao na kujiunga na CHADEMA.

Hata hivyo, mpaka sasa, ni takriban wiki tatu sasa tangu mwanasiasa huyo ahamie CHADEMA na hakuna dalili za yale mafuriko aliyoahidi wakati anajiunga na CHADEMA. Mpaka sasa ni wenyeviti wawili tu wa mikoa wa CCM waliojiunga na Lowasa ilhali aliahidi kuwa zaidi ya nusu ya wenyeviti wa mikoa na wilaya watatangaza kujiunga na CHADEMA. Pia alitangaza kuwa kuna wakuu wa mikoa na wilaya watajiunga na CHADEMA ambapo mpaka sasa, hakuna mkuu wa Mkoa wala wilaya aliyejiunga na CHADEMA.

Pia, hakuna mbunge aliyepitishwa na CCM ambaye ametangaza kujiunga na CHADEMA. Waliojiunga na chama hicho ni wale waliokatwa kwenye kura za maoni kutokana na kushindwa kutimiza matarajio ya wananchi kwenye majimbo yao.

Kwa upande wa wanachama wa kawaida, hapa ndipo hofu ya Lowasa ilipo. Mpaka sasa hakuna lile wimbi la wanachama wa CCM kwenda CHADEMA, baadhi waliokuwa na hasira kutokana na watu wao kukatwa hali imetulia baada ya kuujua ukweli.

Swali la kujiuliza, je Lowasa ameshindwa kufikia dau la kuweza kuwanunua wana CCM zaidi au ameuziwa mbuzi kwenye gunia?

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: