August 19, 2015

Kutoka Diamond: Mapokezi ya Magufuli baada ya kurejesha fomu NEC

Kikwete: CCM haibahatishi, ni chama kikubwa kinawajua watu wake vizuri, sasa nataka nimlete ndugu Magufuli. Anaimbisha wimbo wa kumkaribi... thumbnail 1 summary
Kikwete: CCM haibahatishi, ni chama kikubwa kinawajua watu wake vizuri, sasa nataka nimlete ndugu Magufuli. Anaimbisha wimbo wa kumkaribisha Magufuli. Watu wajue leo CCM ndio imeanza, kama walikuwa wanchukua picha na kuunganisha kwenye computer, sasa zinakuja picha za kweli. John Magufuli ndio Rais na Samia ndio makamu


Magufuli: CCM oyeee, Ali nselema...

Sikutegemea kama patakua na wananchi wakereketwa ndani ya mioyo yao na wenye nyuso za furaha na wamependeza kweli kuhudhuria muda huu. Nimeomba kukutana na wazee wa Dar es Salaam kwa niaba ya wazee wa Tanzania, nafahamu ukitaka kupata busara, utapata kwa wazee. Uzuri leo wazee wamesindikizwa na vijana, ninawashukuru sana. Kabla sijaendelea niwashukuru wazee na wananchi wa Dar kwa kunikaribisha, niliingia mara ya kwanza 1978 wakati naenda kujiunga kidato cha tano, nilikaa siku mbili kisha nikaelekea Iringa. Nilipokuja tena kwa masomo ya chuo kikuu sijawahi kuulizwa dini wala kabila langu. Ninawashukuru sana wana-Dar es Salaam na watanzania.

Ninyi wazee wa Dar mna historia kubwa katika taifa hili, baba wa taifa wakati akiwa kwenye harakati za kudai uhuru alifika Dar es Salaam na akakutaa na wazee, mkamuombea dua na kumbariki na hatimae tukapata uhuru bila kumwaga damu, wakati wa Idd Amin, Nyerere alikutana tena na wazee wa Dar es Salaam, akazungumza nao na mkampa uwezo wa kwenda kushina na yeye akatamka nia tunayo, uwezo tunao. Idd Amin akakimbilia huko alipokimbilia.

Leo wazee wangu nami nimewaita ili nije nipate busara zenu na dua zenu kwa sababu natambua nikizungumza na wazee wa Dar es Salaam mambo yangu yatakua safi kabisa. Mara baada ya kuteuliwa na kupata kura nyingi kabisa na baada ya kumpata Mh Samia kuteuliwa nafasi ya makamu urais kwa mara ya kwanza. Ninachowaomba watanzania na Dar kwa ujumla tuwe wamoja, kura zimeshamalizika, sasa jukumu letu kubwa tulilonalo ni kuhahakikisha tunafanya kampeni nyumba kwa nyuma, kutanda kwa kitanda, uvungu kwa uvungu mpaka tunashinda. Ndugu zangu wa Dar leo haya nilikuwa nachomekea tu, kwa sababu nafahamu tar 23 pale Jagwani itakuwa ndio siku yenyewe ya kuzungumza lakini niwaambie, mimi ninatosha kila mahali. Mbele natosha, nyuma natosha, ubavuni natosha na kila mahali natosha. Shida za wana-Dar es Salaam nazifahamu na kwa bahati nzuri katika uzoefu wa miaka 20 niliokaa serikali, sijawahi kushindwa mahali, mtuamini na hatutawaangusha. Mungu awabariki sana, yatakayokuja kwetu kama changamoto tutayakamilisha kwa nguvu ya hali ya juu. Na vyama vishindwe na vilegee.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: