December 19, 2014

X WA DIAMOND PLATNUMZ,VJ PENNY ATAFUTA MWANAUME WA KUZAA NAYE

Penniel Mwingilwa. Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tat... thumbnail 1 summary


Penniel Mwingilwa.
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.Penny alitoa tamko hilo baada ya 
Diamond kunukuliwa jana (Alhamisi) na gazeti dada la hili, Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi.
“Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: