November 16, 2014

MSANII AJUTIA PENZI LA DK.CHENI

MSANII wa Bongo Movies, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema anajutia kitendo chake cha kumtolea nje staa wa filamu Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Che... thumbnail 1 summary
MSANII wa Bongo Movies, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema anajutia kitendo chake cha kumtolea nje staa wa filamu Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ pale
alipotangaza nia ya kutaka kumposa na kujiona bado mdogo.
Msanii wa Bongo Movies, Fatuma Ayubu ‘Bozi’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Bozi alisema kuwa, miaka mingi iliyopita, akiwa ametoka kuchezwa unyago, mkongwe huyo wa sanaa ya maigizo alitinga nyumbani kwao kwa lengo la kumuoa na kukubaliana na wazazi wake, akamletea pozi.
Staa wa filamu Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’.

“Dah! Sa hizi ningekuwa nimetulia kwenye ndoa yangu na Dk. Cheni sababu wazazi walikubali, sasa maringo yangu yameniponza,” alisema Bozi.Alipotafutwa Dk. Cheni kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kumfahamu Bozi kama msanii lakini hakumbuki kama aliwahi kumtaka.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: