September 07, 2014

NINI MAONI YAKO JUU YA UKAGUZI WA MASHINE ZA EFD?

Ukaguzi wa mashine za EFD umepelekea Wamiliki wa maduka ya bidhaa mbalimbali Kariakoo jijini Dar es salaam kufunga maduka hayo, wali... thumbnail 1 summary


Ukaguzi wa mashine za EFD umepelekea Wamiliki wa maduka ya bidhaa mbalimbali Kariakoo jijini Dar es salaam kufunga maduka hayo, waliamua kuyafunga maduka yao kwa kinachodaiwa kuhofia
ukaguzi wa mashine za EFD yaani(Electronic Fiscal Divices) na mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA), jambo hili lilisababisha mgomo huo kuanza siku chache zilizopita ambapo wengi wa wafanya biashara hao walianza mgomo tarehe 1/9/2014.


Inasemekana kuwa endapo ukaguzi huo ukifanywa na mamlaka ya mapato nchini Tanzania TRA na kukuta mashine hizo zimechezewa, mfanyabiashara husika hurazimika kupigwa faini na mamlaka husika yaani TRA. Hivyo hicho ndicho kilicho wafanya baadhi ya wamiliki wa maduka hayo kuyafunga. 

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: