August 05, 2014

MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE AZINDUA MAKTABA YA KISASA SHULE YA SEKONDARI CHALINZE‏

Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze jana ambayo ime... thumbnail 1 summary

Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze jana ambayo imejengwa na
Kampuni ya Tanga Cement kupitia bidhaa yake ya Simba Cement kwa kushirikiana na taasisi ya Read International kwa gharama ya shilingi milioni 42 za kitanzania katika kuboresha elimu jimboni humo, Mbunge huyo pia ameahidi
kujenga jiko katika shule hiyo na kuongeza kompyuta ili wanafunzi wajengewe mazingira mazuri zaidi ya kujisomea.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni kabla ya kuzindua rasmi maktaba ya shule hiyo, Katikati ni Emma Lyu kutoka taasisi ya Read International na kushoto ni Raquel Araya kutoka Taasisi ya Read International pia.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akionyeshwa vitabu mbalimbali vilivyopo katika maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze na Najma Juma kutoka Chuo Kikuuu cha Dar es salaam UDSM ambaye anafanya kazi za kujitolea katika taasisi ya Read Internional.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akiangalia kitabu wakati akikagua maktaba hiyo kulia kwake ni Najma Juma wa Read International.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akiweka alama za kiganja chake kama kumbukumbu wakati alipozindua maktaba hiyo jana kwenye shule ya sekondari ya Chalinze.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni alipokuwa akisoma risala yake mbele ya mbunge huyo, kutoka kulia ni Raquel Araya kutoka taasisi ya Read International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na wanafunzi wa sule ya sekondari ya Chalinze pamoja na walimu mara baada ya kuzindua maktaba katika shule hiyo jana kushoto ni Mbwana Madeni mwenyekiti wa bodi ya shule, na kutoka kulia ni Raquel Araya kutoka Read International na mkuu wa kituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua maktaba hiyo kushoto ni mdau wa masuala ya habari Dk Fadhil Kabujanta wa Fadhaget Sanitarium Clinic ya Mbezi Africana jijini dar es salaam.
Meneja masoko wa Simba Cement Yasin Hussein akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Maktaba ya shule hiyo iliyojengwa na Kampuni hiyo gharama yake ikiwa ni shilingi milioni 42 za kitanzania.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: