August 24, 2014

Kauli ya Carlo Ancelotti kuhusu Di Maria kuaga wenzake leo hii

Sakata la usajili wa winga wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria kwenda klabu ya Manchester United limechukua sura mpya leo hii. thumbnail 1 summary

IMG_6651.JPG


Sakata la usajili wa winga wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria kwenda klabu ya Manchester United limechukua sura mpya leo hii.

Kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kocha wa Real madrid Carlo Ancelotti amethibitisha mchezaji huyo yupo karibuni kuhama.
Di Maria leo hakufanya mazoezi na wenzake na badala yake alienda kuwaaga wachezaji pamoja na viongozi wengine wa Madrid.
“Alikuja leo asubuhi,
lakini hakufanya mazoezi. Uhamisho wake bado haujakamilika wote ila anakaribia kuhama kabisa.
“Tunamshukuru kwa kila alichoifanyia hii klabu na tunamtakia kila kheri huko anapokwenda, uhamisho haujakamilika rasmi, ila kila kitu tumeshakubaliana,” – Ancelotti alisema.
Ingawa Ancelotti hakuitaja timu anayoenda Di Maria lakini vyombo vya habari ulaya vinaripoti kwamba DI Maria atakuwa mchezaji mpya wa Man united kwa ada ya £64 million.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: