July 25, 2014

TAZAMA PICHA ZA MAITI, AJALI MBAYA HUKO SHINYANGA

Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga thumbnail 1 summary
Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga

Hapa ni katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo majeruhi 29 hadi sasa wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina ya fuso iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Alhamis.Pichani majeruhi waliendelea kuhudumiwa na wataalam wa afya katika hospotali ya mkoa wa Shinyanga

Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel ameiambia malunde1 blog kuwa mpaka sasa wamepokea miili miwili ya marehemu na majeruhi 29
Huduma inaendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga


Baadhi ya majeruhi wameiambia blog Hii kuwa gari aina ya fuso waliyokuwa wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso nyingine na ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka

Kulia ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama barabarani



Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akizungumza na waandishi wa habari hivi punde-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: