July 17, 2014

Je, wivu katika mapenzi unaleta maana?

Assalam Alaikum! Ni furaha yangu kwa mara nyingine tena kukutana nanyi wapendwa wasomaji wa safu yetu hii ya uwanja wa mapenzi. Tumshu... thumbnail 1 summary

Assalam Alaikum! Ni furaha yangu kwa
mara nyingine tena kukutana nanyi
wapendwa wasomaji wa safu yetu hii ya
uwanja wa mapenzi. Tumshukuru Muumba
wetu kwa kutujaalia uhai na afya njema,
lakini zaidi ya hapo tumshukuru pia kwa
kutuumbia kitu mapenzi au sio?
Siku zote hatutaacha kuzungumza juu ya

mapenzi kwani ni ukweli usiopingika
kwamba mapenzi ndio maisha yetu.
Tunafanya kazi usiku na mchana,
tunahangaika huku na huko, lakini mwisho
wa siku tunafikiria jinsi gani tutapata
kuboresha na kufurahia maisha na wapenzi
wetu. Tunafikiria pia ni jinsi gani tunaweza
tukapata utulivu na amani katika maisha ya
kimapenzi na wapenzi wetu, waume zetu
au wake zetu katika siku zote za maisha
yetu.
Wiki hii nimeona ni vyema tukabadilishana
uzoefu juu ya suala zima la wivu katika
mapenzi. Mtakubaliana nami kuwa suala la
kuwa na wivu kwa mpenzi wako ni jambo
lisilokwepeka hasa kwa sababu kubwa ya
kuaminika kwake kwamba kuwa na wivu ni
moja ya kigezo cha kuonesha ni jinsi gani
unampenda mpenzio na kwamba hauko
tayari kwa namna yoyote ile kushea na
mwingine ndio maana wanawake wengi
hawataki kusikia suala la ukewenza
kabisaa! Hata kama jambo hilo limepewa
baraka zote na dini au tamaduni zao.
Lakini kubwa katika wivu ni ile kutokuwa
tayari kuona tunasalitiwa na wapenzi na
hasa kwa wale tunaowapenda ukweli toka
moyoni mwetu na zaidi ukute ndo
tumeshawagharamikia kiasi cha kutosha na
kujitoa kwao kwa kila kitu!
Umeshawahi kusikia kauli kama "Jamani
mke (au mume) anauma! Au kauli kama
mke wa mtu sumu" na hugeuka sumu
kweli hasa pale "unapobambwa" na mali za
wenyewe, kufanyiwa "kitu mbaya" inakuwa
sio jambo la ajabu sana.
Niwaambie kitu wapenzi wasomaji!
Mapenzi bwana ni "full uchoyo, ni full
kujipendelea! Mpenzi wanaume kwa mfano,
anaweza kufikiria kwamba ni yeye tu ndiye
anayestahili na anayeweza kumfanya
mpenzi wake acheke na kufurahi.
Na kwamba akitokea mwanaume
mwingine akapata nafasi ya kumfurahisha
mpenzi huyo hata katika stori za kawaida
tu, unaweza ukasikia akisema, "Hivi wewe
mna nini na huyo jamaa, mbona
unamchekea chekea hivyo, au…!" Hiyo
ndiyo choyo ya penzi, na kikubwa
kinachofanyika hapo ni ile tu kujaribu
kulinda maslahi binafsi.
Pamoja na ukweli kwamba tabia ya wivu
inapozidi hugeuka kuwa kero, lakini kabla
hatujafika huko hebu tuangalie nafasi ya
wivu katika mapenzi yetu. Yaani swali ni
kwamba, je! Wivu katika mapenzi unaleta
maana?
Nionavyo mimi wivu ukitumika vizuri
unaleta maana na una
nafasi muhimu sana
katika mapenzi kwa sababu zifuatazo:
Huonesha kujali
Sote tunaamini pasipo na wivu hata
chembe, hapana mapenzi ya kweli.
Kumuonesha wivu mpenzi wako ni
kumjulisha ni kiasi gani unamjali na
kumpenda na kwamba yeye ni mtu maalum
sana kwako.
Jamani, mahali penye mapenzi yasiyo na
wivu hata kidogo, panatia shaka! Na mara
nyingi majibu yake ni kutokuwa "sirias"
katika uhusiano huo au huenda kuna
kupitisha muda tu na kwamba labda
hakuna "future" na mpenzi huyo au ni dalili
ya kuchuja kwa penzi.
Kuthamini uhusiano
"Sio kama sikuamini dear, bali wivu wangu
kwako ni katika kuuthamini uhusiano wetu,
mimi na wewe ni umoja wenye thamani
kubwa, tusiruhusu kuuchezea nje yetu! Huu
ni mfano wa ujumbe unaoonesha maana
na nafasi ya wivu katika mahusiano ya
kimapenzi.
Kukumbushana
Kauli au matendo yanayoashiria
kumuonesha wivu mpenzio yanasaidia kwa
kiasi kikubwa kumfanya mwenzi wako
"asijisahau" katika jukumu la kulienzi penzi
lenu hata akiwa mbali ya upeo wa macho
yako.
Kujijengea heshima
Kwa namna moja au nyingine, wivu pia
huweza kukujengea heshima. Kwa mfano
mume mwenye wivu na mkewe hujijengea
heshima ya kwamba kweli anamjali na
kumpenda mkewe lakini pia anaweka
mazingira ya
kutosumbuliwa kwa mke
wake huyo kumjengea heshima yake kama
mke wa mtu.
Husaidia kubadilisha tabia
Ukiwa na wivu, unaotokana na mavazi
"tatanishi" anayopendelea kuvaa mpenzi
wako kwa mfano, huenda ikasaidia kubadili
tabia yake.
"Ni kweli umependeza na umetoka "chicha"
ile mbaya mpenzi, lakini mh! Naogopa
wanaume wakware watakusumbua honey,
unaonaje ukavaa simpo tu?" Kama
anakupenda huenda akabadilika kidogo na
hivyo "vivazi vyake". 

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: