June 24, 2014

UHOLANZI HAWANA MCHEZO KOMBE LA DUNIA WAICHAKAZA CHILE KWA SHIDA

LOUIS van Gaal ameiongoza Uholanzi kupata ushindi wa asilimia 100 katika kundi B baada ya Leroy Fer na Memphis Depay wakitokea benchi... thumbnail 1 summary

LOUIS van Gaal ameiongoza
Uholanzi kupata ushindi wa
asilimia 100 katika kundi B baada
ya Leroy Fer na Memphis Depay
wakitokea benchi kufunga mabao
mawili dhidi ya Chile usiku huu.
Kiungo wa Norwich City , Fer
alifunga bao lake katika dakika ya
77 ikiwa ni dakika mbili tu tangu

aingie, naye Depay alifunga bao la
pili dakika ya 92 akimalizia krosi
ya Arjen Robben na kuipa Uholanzi
ushindi huo wa mabao 2-0.
Kikosi cha Uholanzi: Cillessen,
Blind, Vlaar, De Vrij, Kuyt (Kongolo
89), De Jong, Wijnaldum, Janmaat,
Sneijder (Fer 75), Lens (Depay 69),
Robben.
Wachezaji wa
akiba: Vorm, Martins
Indi, de Guzman, Verhaegh,
Veltman, Clasie, Huntelaar, Krul.
Kadi nyekundu: Blind.
Wafungaji: Fer 77, Depay 90+2.
Kikosi cha Chile: Bravo, Silva
(Valdivia 70), Medel, Jara, Isla,
Aranguiz, Diaz, Mena, Gutierrez
(Beausejour 46), Vargas (Pinilla 81),
Alexis.
Wachezaji wa akiba: Toselli,
Albornoz, Carmona, Vidal, Rojas,
Orellana, Fuenzalida, Paredes,
Herrera.
Kadi ya njano: Silva.
Mwamuzi: Bakary Gassama
(Gambia)

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: