June 26, 2014

JWTZ kuanika tena zana zake za Kivita jijini Dar katika kongamano kubwa la kijeshi....

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajiwa kufanya maonesho ya zana zake za kivita zinazotumiwa na askari wa nchi kav... thumbnail 1 summary

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) linatarajiwa kufanya maonesho ya
zana zake za kivita zinazotumiwa na askari
wa nchi kavu kuanzia Julai 14 hadi 16,
mwaka huu wakati wa kongamano kubwa
la kijeshi ambapo ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwa jeshi hilo nchini.
Kampuni zaidi ya 30 zinazotengeneza silaha
na vifaa vya kijeshi kutoka ndani na nje ya
nchi zitaonyesha bidhaa zao katika

Kongamano hilo.
Akizungumzia kongamano hilo
litakalofanyika kwenye Ukumbi wa wa
Milimani City, Dar es Salaam, Julai 14 hadi 16,
mwaka huu, mkuu wa kamandi ya Jeshi la
Nchikavu, Meja Jenerali Salim Kijuu alisema
jana kuwa viongozi mbalimbali wakiwemo
wadau wa jeshi watashiriki.
"Kampuni 32 za kimataifa zinazozalisha na
kuuza silaha na vifaa vya kijeshi
zimethibitisha kushiriki katika maonyesho
hayo. Viwanda vyetu vya kijeshi na
vile vya
kiraia vinavyozalisha silaha za kijeshi pia
vitashiriki," alisema Kijuu.
Alibainisha kuwa Tanzania itatumia fursa
hiyo kulitangaza jeshi lake katika jumuiya za
kimataifa, hasa katika kipindi ambacho
linaelekea kwenye maadhimisho ya miaka
50 tangu lilipoanzishwa.
Alisema majeshi yatakutana kujadili jinsi ya
kukabiliana na changamoto za sasa za
ulinzi na usalama hasa eneo la Afrika
Mashariki ambalo linakabiliwa na
changamoto ya uvuvi haramu, uharamia na
jinsi ya kulinda maliasili za Taifa.
Brigedia Jenerali Simon Mumwi alisema
ingawa maonyesho hayo yanahusu silaha
na zana za
kijeshi, hayana lengo la kuzitisha
nchi jirani, bali kuimarisha uhusiano.
"Tunawaalika wenzetu ili waje tupeane
ujuzi na uzoefu wa changamoto za
kiusalama na siyo kuwaonyesha kwamba
na sisi tupo," alisema Mumwi.
Kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50
ya JWTZ Agosti, mwaka huu, kutafayika
mazoezi makubwa ya kijeshi Arusha.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: