June 11, 2014

EXCLUSIVE VIDEO: KUTOKA KWA FLORA MBASHA AKIMUELEZEA MUME WAKE ALIVYOBAKA,

Taarifa kuhusu tuhuma za mume wa mwimbaji wa injili Flora Mbasha kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 ziliwashitua wengi na kuacha ma... thumbnail 1 summary

Taarifa kuhusu tuhuma za mume wa mwimbaji wa injili Flora Mbasha kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 ziliwashitua wengi na kuacha maswali ya nini kilitokea na nini kilipelekea.


Flora Mbasha ni mmoja kati ya waathirika wa tetesi za kuwa chanzo cha kuiporomosha ndoa yake ameelezea tukio na yaliyofanyika kabla ya kutokea (Mazingira ya awali).

Mwimbaji huyo ameeleza kuwa hakuwa anamuelewa mume wake kwa muda mchache kabla ya kwenda ibadani ambapo alikataa kumpa gari la kwenda nalohuku akimporomoshea matusi makali ya nguoni kiasi cha kuhisi labda kapigwa kipapai, “niliimuliza mume Mbasha au umerogwa mume wangu?”.
Baada ya wa ibada umekaribia, alipigiwa simu mchugaji Gwajima na akatumiwa gari ili aende kanisani na famili ya mchungaji kitu ambacho kikimuongeza hasira mumewe ambaye alipiga simu na kuendelea kumtukana.

Anadai kuwa mume wake alifikia hatua ya kumkaba shingoni kama jinamizi vitendo ambavyo kwake
havikuwa vya kawaida huku akimtishia kumuua.
Siku moja baadae binti waliyekuwa wanaishi nae nyumbani alianza kulalamika kuhusu tukio alilofanyiwa na Emmanuel Mbasha, tukio la kidhalilishaji na kinyanyasaji na taarifa zilimfikia Flora ambaye alikuwa hotelini muda huo.


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: