April 07, 2014

TIMU YA WATOTO YA TANZANIA IMEINGIA FAINAL KOMBE LA DUNIA LA WATOTO WA MITAANI

Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imefanikiwa kuingia fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada thumbnail 1 summary
Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imefanikiwa kuingia fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada
ya kuifunga Marekani goli  6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janeiro Brazil.
Mpaka timu zinaenda mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa goli 4-0,goli pekee la Marekani katika mchezo huo ambayo hadi nusu fainali ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za mwisho za mchezo huo.
Kwa matokeo haya Tanzania inacheza nusu fainali na Burundi,Mechi hiyo inachezwa leo (Aprili 6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Pakistan goli 4-3 katika nusu fainali ya pili.

Mchezo huo wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi  akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza George Osborne.
Katika mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo,Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: