Mwanamuziki na mwigizaji nyota wa muziki wa Dansi Patcho Mwamba amesikitishwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitafuta
umaarufu kupitia majina ya watu japo kwa kufanya hivyo ni kitu kinachoumiza familia za wanaotendewa hivyo, akitolea mfano kwa mtu anayejiita mchungaji George Kairuki ambaye amekuwa akitumia jina la marehemu Kanumba.
Anatangaza vitu vya uongo eti Kanumba alikuwa Freemason kitu cha uongo kabisa, marehemu Kanumba alikuwa rafiki yangu na mtu wa karibu hakuwa mtu wa ajabu, unaweza kupata kesi kwa mwendawazimu kama huyo,”anasema Patcho.
Source:pro-24