April 04, 2014

HEMEDY "KINA DADA MNIACHE SITAKI KUFUATWA FATWA MMENISUMBUA KWA KIPINDI KIREFU"

STAA wa filamu za Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’, amewataka kina dada wanaomtaka mahusiano ya kimapenzi kukaa thumbnail 1 summary
STAA wa filamu za Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’, amewataka kina dada wanaomtaka mahusiano ya kimapenzi kukaa
mbali naye, kwani kwa sasa ameamua kutulia na mpenzi wake, na anatarajia kufunga ndoa.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, PHD aliandika kuwa kwa sasa yupo tayari kumweka hadharani mpenzi wake, ambaye anatarajia kufunga naye ndoa hivi karibuni, hivyo hataki kufuatwa na wasichana ambao hawapendi maendeleo yake.

“Nimekuwa nikisumbuliwa sana kwa kipindi kirefu, hata mimi pia nimewachezea sana watoto wa watu, sasa nimeamua kutulia na kuwa mwanaume bora, maana nimegundua nilikuwa nafanya ujinga, umri ushaenda, natakiwa niwe na familia yangu,” aliandika.
Mbali na hilo,

PHD alisema yupo katika hatua za mwisho za maandalizi ya video ya ngoma yake mpya anayotarajia kuisambaza mwezi huu inayojulikana kwa jina la ‘On My Wedding Day’.
Alisema katika wimbo huo, amezungumzia mambo mengi ambayo anatarajia yatakuwepo siku yake ya harusi, hivyo anaomba sapoti kwa mashabiki ili iweze kufanya vizuri.
PHD ni kati ya nyota wa Bongo wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu na muziki, kutokana na ubora wa kazi zake na anavyoweza kucheza uhalisia mbele ya kamera.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: