May 28, 2014

NI HUZUNI TANZANIA KWA KUMPOTEZA MSANII MKONGWE MZEE GURUMO NA LEO NDIO AROBAINI YAKE 40 TUSISAHA

UNAFIKI  kwa mastaa wa Bongo unaendelea kujidhihirisha ambapo safari hii wamekacha dua ya arobaini ya nguli wa muziki wa dansi nchini, Mu... thumbnail 1 summary
UNAFIKI kwa mastaa wa Bongo unaendelea kujidhihirisha ambapo safari hii wamekacha dua ya arobaini ya nguli wa muziki wa dansi nchini, Muhidini
Gurumo, shughuli iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Mabibo, Dar, Jumamosi iliyopita.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria 40 Gurumo.
Waandishi wetu walishuhudia wanamuziki wa Msondo Ngoma, Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka na wengineo wachache wakiwa kwenye shughuli hiyo, bila ya mastaa kama ilivyotarajiwa na wengi.
Akizungumzia ishu hiyo, Asha alisema mastaa wa Bongo ni wanafiki na wanapenda kuuza sura ndiyo maana hutokea kwa wingi siku ya mazishi wakijua kuwa vyombo vya habari huja kwa wingi.
Maalim Gurumo enzi za uhai wake.
“Wasanii na mastaa wetu wanatia aibu. Utakuta kunatokea tatizo, wala hawaendi, wanasubiri mazishi ili wajipitishe mbele ya kamera. Sasa angalia kwa staa mkubwa kama mzee Gurumo, ni sahihi kuhudhuriwa na watu wachache namna hii?
Wakina mama wakiwa kwenye arobaini hiyo.
“Mbaya zaidi mastaa hawaonekani wakati kwenye msiba walilia na kusema wana uchungu
na mzee wetu. Wasanii wasijisahau, wanatakiwa kushirikiana na wenzao katika hali na mali, nazungumzia wote,  wasanii wote wa Bongo Fleva na Bongo Muvi,” alisema Asha.
Katika hatua nyingine, mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye  Mwalimu Muhidini Gurumo, alikanusha habari zilizoenea kuwa wana mpango wa kuuza nyumba yao.
Arobaini ikiendelea nyumbani kwa marehemu Gurumo.

“Huo ni uzushi, hatuwezi kugawanyika kisa mali za baba, kwa mfano hii nyumba yetu hatuiuzi kabisa kwa sababu ndiyo kumbukumbu pekee iliyobaki kuhusu mzee wetu, hapa wageni wote ndipo wanapofikia, sasa kwa nini tuuze? Si kweli,” alisema.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: