MSANII wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amesema hivi karibuni aligongana uso kwa uso na Ivon Bigilwa ambaye anadaiwa kumchana kwa chupa
mkononi na kesi hiyo inaendelea katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Msanii wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel akliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
Aunty alisema hayo juzi Jumatatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya hakimu Agustina Mbando, akikanusha taarifa ya wadhamini wa Ivon, Christopher Mwaseba na Anthon Mwaseba walioiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alikuwa nyumbani akimuuguza mama yake.
Msanii huyo alisema wadhamini hao wanaidanganya mahakama kwa kuwa hivi karibuni alikuwa nchini China na aligongana naye uso kwa uso.