May 28, 2014

Mbio za mwenge wa uhuru na gharama zake….

Bunge la bajeti linaendelea Dodoma Tanzania ambapo jana May 27 2014 kwenye kipindi cha maswali na majibu asubuhi, moja ya majibu yaliyot... thumbnail 1 summary

mwenge

Bunge la bajeti linaendelea Dodoma Tanzania ambapo jana May 27 2014 kwenye kipindi cha maswali na majibu asubuhi, moja ya majibu yaliyotolewa ni kuhusu
uwepo wa mbio za mwenge na gharama zake. 
Naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia amesema serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika ambapo mwaka 2012 jumla ya shilingi milioni mia sita hamsini (650) zilitengwa kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kati ya hizo milioni 450 zilitumiwa na Wizara na milioni 200 zilitumiwa na mkoa uliokua mwenyeji wa sherehe za kilele
Kuhusu kiasi cha fedha kinachotumiwa na wilaya, ni kwamba zinatofautiana kulingana na michango ya Wananchi katika wilaya husika kwani michango hiyo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo huzinduliwa wakati ya mbio za mwenge, kwa ujumla mwaka 2012 Wananchi walichangia zaidi ya Bilioni  11 na milioni 500.
Halmashauri za wilaya na manispaa zilichangia shilingi Bilioni 45, Wahisani na watu binafsi walichangia zaidi ya shilingi milioni 52 ambapo faida zinazopatikana kutokana na Mwenge wa Uhuru nchini ni pamoja na kuendelea kutunza historia na falsafa ya ukombozi wa taifa letu, kuhamasisha Wananchi kuhusu umuhimu wa kuendelea kuenzi amani, mshikamano, upendo na zaidi kupambana na ubaguzi wa dini, rangi au ukabila
Mbio za mwenge wa uhuru hutumika kuhimiza miradi mbalimbali kwa njia ya kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyowekewa jiwe la msingi mwaka uliopita na pia kuhamasisha moyo wa Wazalendo na kujitolea kwa vijana hasa kuonyesha umuhimu na nafasi yao katika kudumisha nchi yao, kulinda uhuru na kuleta maendeleo ya nchi yao

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: