October 28, 2015

WABUNGE NA MADIWANI WOTE, CCM NA UKAWA WALIOKWISHA KUTANGAZWA RASMI ..KUANZIA TAR;25-27 MDA HUU..JE KUNA UWEZEKANO WA SERIKALI MSETO?

Tunawaletea matokeo rasmi kwa nafasi ya Ubunge kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yanavyotangazwa na Wakurugenzi wenye dha... thumbnail 1 summary
Tunawaletea matokeo rasmi kwa nafasi ya Ubunge kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yanavyotangazwa na Wakurugenzi wenye dhamana hiyo 

Tembelea ukurasa huu mara kwa mara kwa updates zaidi

Jimbo la Magu: Kiswaga Boniventura wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 61508 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ngongoseke Julias wa Chadema, aliyepata kura 32217 

Jimbo la Busanda, mkoani Geita Lolesia Bukwimba mgombea toka Chama cha Mapinduzi(CCM) atangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge kwa kupata jumla ya kura 63,043 huku mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Mawazo Alphonce kupata jumla ya kura 45,019 

Jimbo la Kilwa Kaskazini, mkoani Lindi kupitia tiketi ya CUF Ngombare Edgar ameibuka kuwa mshindi kwa kupata jumla ya kura 16,724. Huku mpinzani wake toka Chama cha Mapinduzi (CCM) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 16,303 

Jimbo la Sengerema: William Ngeleja wa CCM, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 49877, dhidi ya mpinzani wake karibu Tabasam Mwagao wa Chadema, aliyepata kura 36281 

Jimbo la Buchosa: John Tizeba wa CCM, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 59971, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Michael Kaswahili wa Chadema, aliyepata kura 35023 

Jimbo la Kilolo: Vinance Mwamoto wa CCM, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 45227, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Kikoti Bryson wa Chadema, aliyepata kura 32926 

Jimbo la Kwimba: Mansoor Hirani wa CCM, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 39857, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Shilogela Nganga wa Chadema, aliyepata kura 7338 

Jimbo la Mikumi: 
Jimbo la Mikumi: Joseph Haule wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 32259, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Nkya Estomih wa CCM, aliyepata kura 30425. 

Updates:Mabasi mawili ya Kampuni ya Zacharia Express yanayofanya safari zake Tarime-Mwanza yameharibiwa kwa kupondwa na mawe jana mchana kwa kile kinachoelezwa ni ushabiki wa kisiasa, taarifa ya polisi yasema.

Updates:Ubunge Nyamagana Wapingwa: Mgombea wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Wenje amepinga matokeo ya jimbo hilo baada ya kushindwa huku akilalamika kuibiwa kura kwa sababu taratibu za kuhesabu zilikiukwa.

Updates:Ubunge Mbagala: Fomu 104 za matokeo katika jimbo la Mbagala zinadaiwa kutoonekana huku fomu 84 ndizo zinazoonekana,hali hiyo imepelekea kuwapo kwa malalamiko mengi kutoka kwa mawakala wa vyama vya siasa. 
Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki: Omary Mgumba wa CCM ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 27940, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Salama Awadh wa CUF, aliyepata kura 13823 

Jimbo la Wanging'ombe mkoani Njombe mgombea wa CCM Gerson Hosea Lwenge ameibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake wa karibu Disman Andrea Luhwago wa CHADEMA 
Jimbo la Muhambwe – Kigoma Atashasta Justus Nditiye ameshinda Ubunge kwa tiketi ya CCM, na kumbwaga mpinzani wake wa NCCR Felix Francis Mkosamali katika kinyang’anyiro hicho 
Updates: Lazaro Nyalandu ameibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha ubunge jimbo la Singida Kaskizini kwa tiketi ya CCM kwa kupata kura 42,191, Huku Mpinzani wake wa CHADEMA David Joseph Mghanja akipata kura 20,264 
Updates:Jimbo la Rungwe mgombea wa CCM Saul Henry Amon ameshinda ubunge kwa kura 44,745, huku mpinzani wake wa CHADEMA kapata kura 43,613 John David Mwambigija. hivyo CCM kuibuka mshindi katika kiti hicho 

Updates:Mgombea ubunge wa jimbo la Ileje kwa tiketi ya CCM Janet Zebebayo Mbene ameibuka mshindi kwa kujinyakulia kura 27582 dhidi ya kura 14578 za mpinzani wake wa karibu Emmanuel Amanyisye Mbuba wa NCCR 
Updates:Mgombea wa kiti cha ubunge kupitia tiketi ya CCM kwenye Jimbo la Busokelo – Mbeya Atupele Fredy Mwakibete aibuka kidedea na kuwa Mbunge mtarajiwa kwa kupata jumla ya kura 20,206. Huku mpinzani wake wa CHADEMA Boniface Anyisile Mwabukusi kushindwa kwa kupata jumla ya kura 12,807 


Updates:Mgombea ubunge wa jimbo la Mbozi mkoani Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA Pascal Yohana Haonga ametangazwa mshindi wa kiti hicho kwa kujinyakulia kura 32442 dhidi ya kura 17220 za mpinzani wake wa karibu Godfrey Weston Zambi wa CCM 

Updates:Harrison George Mwakyembe ameibuka Mshindi wa ubunge katika Jimbo la Kyela kupitia tiketi ya CCM kwa kupata kura 44,269 dhidi ya mpinzani wake Hebel Abraham kwa kura 39,379 

Updates:Mgombea ubunge wa jimbo la Mbarali kupitia tiketi ya CCM Haroon Mulla Pirmohamed ameibuka mshindi wa kiti hicho kwa kura 45352 dhidi ya kura 36603 za mpinzani wake wa karibu Liberatus Laurent wa CHADEMA 

Updates:Mgombea ubunge jimbo la Momba kwa tiketi ya CHADEMA David Ernest Silinde ameibuka mshindi kwa idadi ya kura 26468 huku mpinzani wake wa karibu Luka Jelas Siyame wa CCM akiambulia kura 26260 

Updates:Mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya Vijijini kupitia CCM Oran Manase Mteza ameibuka mshindi kwa kujinyakulia kura 56307 wakati mpinzani wake wa karibu Adam Abraham Zella wa CHADEMA akijinyakulia kura 52298 

Updates:Jimbo la Ubungo- Dar es Salaam Mgombea wa CHADEMA Kubenea Saed Ahmed ameibuka kidedea kwa kujinyakulia kura za Ubunge 87,606 dhidi ya mpinzani wake Massaburi Didas John wa CCM aliyepata kura 59,514 

Updates:Peter Lijuakali (Chadema) ametangazwa kuwa Mbunge Mteule wa jimbo la Kilombero. 

Updates: Suzan Limbweni Kiwanga (Chadema) ametangazwa kuwa Mbunge Mteule wa jimbo la Mlimba 

Updates: Majira ya Saa kumi na nusu alfajiri. Waitara Mwita wa CHADEMA ametangazwa kunyakua kiti cha Ubunge Ukonga, kwa kumbwaga Jerry Slaa wa CCM ambaye alikuwa mpinzani wake mkubwa. 
Jimbo la Bagamoyo: Dk Shukuru Kawambwa (CCM) 26,434, Andrew Kasambala (CUF) 16,330, Mwamini Saidi (UMD) 418 na Saidi Athman (ACT Wazalendo) 418. 


Jimbo la Ngara: Alex Gashaza (CCM) 53,387, Dk Bujari Simon (Chadema) 35,254, Helen Gozi (NCCR-Mageuzi) 997 na Dotto Jasson Bahemu (ACT Wazalendo) 440. 

Jimbo la Msalala: Ezekiel Maige (CCM) 36,010, Paulo Malaika(Chadema) 20, 124, Marco Suwa (ACT Wazalendo) 672 na Abeid Ibeshi (UDP) 251. 

Jimbo la Busega: Dk Raphael Chegeni (CCM) 40,977, David William (Chadema) 26,995 na Zangi Robart (UDP) 802. 

Jimbo la Mbogwe: Augustino Masele (CCM) 32,921, Nicodemus Maganga (Chadema) 13,975 na Andrew Mnuke (ACT Wazalendo) 5,464. 

Jimbo la Bukombe: Dotto Biteko (CCM) 47,147, Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema) 29,929 na Dick Bagamba (ACT Wazalendo) 1,673. 

Jimbo la Babati Mjini: Pauline Gekul (Chadema) 21,970 na Kisyeri Chambiri (CCM) 16,434. 

Jimbo la Kahama Mjini: Jumanne Kishimba (CCM) 47,553, James Lembeli (Chadema) 30,122 na Bobson Wambura (ACT Wazalendo) 605. 

Jimbo la Kibaha Mjini: Silvestry Koka (CCM) 31,462, Paul Mtally (Chadema) 24,860, Habibu Mchange (ACT Wazalendo) 3,438, Gombati Waziri (CCK) 259, Betha Mpata (APPT), 120 na Kibona Ally (AFP) 108. 

Jimbo la Geita Mjini: Kanyasu John (CCM) 34, 953, Rogers Ruhega (Chadema) 26, 303 na Malebo Michael (CUF) 625. 

Jimbo la Mkinga: Dustan Kitandula (CCM) 21,623, Bakari Kassimu (CUF) 13, 547, Rachel Sadick (Chadema) 3,789 na Ali Mwita (ACT Wazalendo) 402. 

Jimbo la Lindi Mjini:Selemani Kaunje (CCM) 20,733 na Salum Barwany (CUF) 18, 843 

Jimbo la Same Mashariki: Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amemshinda Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539. 

Updates: Mgombea Ubunge Jimbo la Mwanga Prof. Jumanne Maghembe wa CCM ameibuka kidedea na kutetea kiti chake cha Ubunge 
-Amembwaga Henry Kileo wa CHADEMA 

Updates: Wilfred Lwakatare (Chadema) kapata kura 28, 112 na kumshinda Balozi Khamis Kagasheki (CCM) aliyepata kura 25, 565 
Updates:Jimbo la Vunjo, Kilimanjaro; Mgombea wa NCCR Ndg. James Mbatia, ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa kura 60,187 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Innocent Melleck Shirima aliyeambulia kura 16,097. 


Updates:Jimbo la Moshi Vijijini, Kilimanjaro; Mgombea wa CHADEMA Anthony Calist Komu ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa jumla ya kura 55,813, akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Dr. Cyril Chami ambaye pia alishawahi kuwa Waziri Viwanda na Biashara aliyepata kura 24,415.

Updates:Jimbo la Nyamagana, Mwanza: Mgombea wa CCM, Mabula Stanslaus Shing'oma ameshinda kwa kuzoa kura 81,017, akifuatiwa kwa karibu na Ezekiel Wenje wa CHADEMA aliyeambulia kura 79,280.

==>CCM pia imeshinda Kata 14 kati ya 18 za udiwani katika Jimbo la Nyamagana huku Chadema kikiambulia Kata Nne, hivyo CCM itaunda Halmashauri ya Nyamagana. 


Updates:Jimbo la Tarime vijijini, mkoani Mara: Mgombea wa CHADEMA, Heche John Wegesa ameibuka kidedea kwa kupata kura 47,249, huku akifuatiwa kwa karibu na Kangoye Christopher Ryoba wa CCM aliyepata kura 42325. 

Updates:Jimbo la Chato, mkoani Geita: Mgombea wa CCM, Dr. Kalemani Matogolo Medard ameibuka mshindi kwa kupata kura 78,817 akifuatiwa na Lukanima Benedicto Kulwizira wa CHADEMA aliyepata kura 32,513. 

Updates:Mgombea wa CCM katika jimbo la Ilala, jijini Dar es salaam, Azzan Mussa Zungu ameibuka kidedea kwa kupata kura 35,818 dhidi ya kura 32,533 za Muslim Haiderali Hassanali wa CHADEMA 


Update: Mgombea ubunge jimbo la Kasulu mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Moses Machali amepoteza jimbo hilo, ameshindwa na Mgombea wa CCM Daniel Sanze.
-Amepata kura 22,512 na mshindi Daniel wa CCM amepata kura 25,336

Updates:Matokeo ya ubunge Iringa Mjini kutangazwa kesho baada ya kuchelewa kupatikana kwa matokeo ya kituo cha Kata ya Ruaha. 

Updates:Jimbo la Sumbawanga Mjini: Aeshi Hilaly wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41763, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ikuwo Malila wa Chadema, aliyepata kura 36183. 

Updates:Joram Hongoli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe kwa kupata jumla ya kura 20,430 na kumwangusha mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Edwin Swalle aliyepata jumla ya kura 10407 

Updates: Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata kura 13665 


Updates:Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa Chadema, aliyepata kura 13480 



Updates:Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM, aliyepata kura 18614. 

Updates: Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema, aliyepata kura 16702 
Updates:Wiliiam Lukuvi ametangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge toka tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ismani, mkoani Iringa kwa kuwa na jumla ya kura 26,119 na mpinzani wake Patrick Sosopi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 15,534

Updates:Jimbo la Mtama: Nape Nnauye wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 28110, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa Chadema, aliyepata kura 13918 
Updates: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215 


Updates:Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa Chadema, aliyepata kura 15347 

Updates: Jimbo la Same Mashariki:Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539

Updates:Jimbo la Ilemela jijini Mwanza Angelina Mabula wa chama cha Mapinduzi CCM ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Hainess Kiwia kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshindwa kukitetea kiti chake 


Updates:Mtwara mjini Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshindwa kukitetea kiti chake 

Updates:Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966. 


Updates:Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyengo Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894 


Updates:Jimbo la Kigoma Mjini: Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 31546, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Amani Kaburou wa CCM, aliyepata kura 16344

Updates:Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 54660, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa Chadema aliyepata kura 12580

Updates:Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 14578 

Updates:Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas Kalinde, aliyepata kura 18649 



Update: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini.

Upadate: Jumanne Kishimba (CCM) ameshinda Jimbo la Kahama Mjini, Steven Masele ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini.

Update: Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini 

Jimbo la Serengeti 
Marwa Ryoba (Chadema) amengazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kupitia tiketi ya Chadema katika jimbo la Serengeti.Jimbo hilo lilikuwa chini ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe 
Jimbo la Chalinze 
Ridhiwani Kikwete wa CCM, aibuka mshindi katika Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani kwa jumla ya kura 52695, dhidi ya Mang’unda Torongei wa Chadema aliyepata kura 23470 

Jimbo la Moshi Mjini 
Japhary Michael wa Chadema ameshinda kwa kura-51647, huku mpinzani wake Davies Mosha wa CCM akipata kura-26920 


Jimbo la Bunda
Wassira aangushwa!
Ni baada ya Esther Bulaya wa Chadema kuchukua Jimbo la Bunda KWA KURA 26207, huku Wassira kupata kura 17573.



Jimbo la Peramiho 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peremiho kwa tiketi ya CCM , Jenister Mhagama ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo 


Jimbo La Arumeru Mashariki 
Mgombea Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema , Joshua Nassari ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo

Nassari ameshinda kwa kura 86694, na mpinzani wake wa karibu John Pallangyo wa CCM amepata kura-31847 

Jimbo la Shinyanga 
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi 


Jimbo la Tandahimba 
Katika jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Katani Ahmed Katani wa CUF ameshinda kiti cha ubunge kwa kura-55156, huku mpinzani wake mkubwa wa CCM, Shaibu Salimu Likumbo akipata kura-41088 



Jimbo la Mbinga Mjini 
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Mjini Sixtus Mapunda ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo 

Jimbo la Musoma Mjini 
Ubunge: Vicent Nyerere(Chadema) 25,549 na Vedastus Mathayo(CCM) 32,836. 


Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Musoma Mjini Vedastus Mathayo ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo 


Jimbo la Mbinga Vijijini 
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Vijijini Martin Msuha ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Monduli 
Ubunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925. 


Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, Ndugu Julius Kalanga ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo 




Jimbo la Siha 
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.

Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).

Jimbo la Tunduma 
Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319. 

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo. 


Jimbo Buyungu 
Ubunge: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934

Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041. 


Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo 


Jimbo la Tarime Mjini 
Ubunge: Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356. 
Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemtangaza Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo

Jimbo la Lindi Mjini 
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: