Usiku wa Jumatano ya October 27 kulikuwa hakuna mechi za Ligi Kuu Uingereza ila ilikuwa ni siku ambayo michezo ya ya Kombe la Capital One iliendelea nchini Uingerezakwa mechi kadhaa kupigwa katika viwanja
mbalimbali Uingereza, moja kati ya mchezo wa Kombe hilo uliyochezwa ni Sheffield Wednesday walicheza dhidi ya Arsenal.
Licha ya klabu ya Arsenal kuwa na mwenendo mzuri katika mechi za Ligi Kuu Uingerezamsimu huu, haikufanikiwa kupata matokeo mazuri mbele ya Sheffield Wednesday, klabu ya Arsenal ilikubali kipigo cha goli 3-0, katika mchezo huo dhidi ya timu ya Sheffield Wednesday ambayo inashiriki Championship.
Magoli ya Sheffield Wednesday yalifungwa na Ross Wallace dakika ya 28 ya mchezo kabla ya dakika ya 40 Lucas Joao kupachika goli la pili, goli ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal kutafuta goli za kusawazisha ila Sam Hutchinson akaongeza goli la tatu dakika ya 52, goli ambalo liliwakatisha tamaa Arsenal ya kupata matokeo mazuri.
Matokeo ya mechi nyingine za Capital One zilizochezwa usiku wa October 27
Video ya magoli ya Sheffield Wednesday Vs Arsenal