August 10, 2016

Waziri wa Magufuli ataka alipwe bilioni moja na gazeti la Mseto

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amelitaka gazeti la Mseto kumuomba radhi na kumlipa fidia ya shilin... thumbnail 1 summary
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amelitaka gazeti la Mseto kumuomba radhi na kumlipa fidia ya shilingi bilioni moja kwa kosa la kuandika habari iliyomchafua.


Waziri Ngonyani amesema Agosti 4 mwaka huu gazeti hilo liliandika habari iliyomhusisha kupokea fedha kutoka moja ya Kampuni ya Madini wakati akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) yenye kichwa kilichosomeka ‘Waziri amchafua JPM’.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake, Waziri Ngonyani amesema, “Nimewaandikia notisi ya siku saba ikiwataka waombe radhi na kunilipa fidia, na wasipofanya hivyo hatua stahiki kuwapeleka mahakamani akiwemo mwandishi Josephat Isango, Mwanahalishi Publisher na Mchapaji wa gazeti hilo.”

Aidha Waziri huyo amekana tuhuma hizo kwa madai kuwa mwandishi wa gazeti hilo ametumia nyaraka za kugushi ikiwemo barua iliyoandikwa tarehe 24 Julai na kutiwa saini yake akiwa Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO wakati ukweli ni kwamba tarehe hiyo yeye alikuwa ni Mkurugenzi kamili na siyo Kaimu kama barua hiyo inavyosomeka.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments