June 01, 2016

Zlatan Ibrahimovic huenda akarudi kwao kumaliza soka lake

Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic matumani ya kucheza soka nchini England msimu ujao, yameingia dosari... thumbnail 1 summary
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic matumani ya kucheza soka nchini England msimu ujao, yameingia dosari kufuatia kauli aliyoitoa usiku wa kuamkia hii leo alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari.


Mshambuliaji huyo ambaye amemaliza mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG, amelidhihirisha wazi kuihusudu klabu iliyomkuza ya Malmo FF ya nchini kwao Sweden.

Ibrahimovic, alisema angependa kuitumikia tena klabu hiyo, kutokana na mapenzi yake ya dhati kuelemea Malmo FF ambapo anapachukulia kama nyumbani kwake.

“Ninaipenda Malmö na ningependa kuitumikia hata hii leo,” alisema Zlatan

“Ninaomba radhi kwa kauli hiyo, lakini ninatarajia na kutarajia. Ila ninaomba kuweni na subra kuhusu hatma yangu.” aliongeza

Hatua hiyo imewaacha wadadisi wa soka barani Ulaya katika hali ya sito fahamu, na kuanza kuhisi huenda mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, akawa na mipango mingine tofauti ya kucheza soka lake utakapofika msimu wa 2016-17.

Meneja mpya wa Man Utd, Jose Mourinho amekua akitajwa kama kivutio kikubwa cha Ibrahimovic kujiunga na klabu hiyo ya Old Trafford, na ilifikia wakati walianza kuhisi huenda angekua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mreno huyo.

Klabu ya Malmo FF ndo iliyo kuwa imkimlea na kumuendeleza kisoka Ibrahimovic na ilipofika mwaka 1999 ilimpandisha katika kikosi cha kwanza ambapo alidumu hapo hadi mwaka 2001, na kuuzwa kwenye klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments