June 01, 2016

Kutumbuiza zaidi ya masaa matatu kwangu ni kama zoezi tu – Ruby

Diva mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Ruby amesema yeye kuimba kwa zaidi ya masaa matatu jukwaani kwake ni kama zoezi tu. Akiongea k... thumbnail 1 summary
Diva mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Ruby amesema yeye kuimba kwa zaidi ya masaa matatu jukwaani kwake ni kama zoezi tu.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Ruby alisema, “Mimi naweza kuperform masaa matatu.”

“Nimekuwa nafanya hivyo kabla sijaingia kwenye bongo fleva nimeanza kuimba live kanisani, tunaperform zaidi ya masaa matatu na masaa matatu kwangu ni kama kufanya mazoezi,” aliongeza.

Wimbo wake ‘Forever’ ni moja kati ya nyimbo zinazofanya vizuri kwenye redio na mbalimbali japo bado video ya wimbo huo haijatoka.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments