June 11, 2016

VIDEO: Ufaransa wamefanikiwa kuanza kwa ushindi Euro 2016 katika ardhi yao

Mtu wangu wa nguvu najua ulikuwa ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanasubiria michuano ya Euro 2016 kufanyika, hiyo inatokana na mvuto wa ... thumbnail 1 summary
Mtu wangu wa nguvu najua ulikuwa ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanasubiria michuano ya Euro 2016 kufanyika, hiyo inatokana na mvuto wa mashindano hayo kukusanya nyota mbalimbali kupitia timu zao za taifa.

June 10 2016 Ufaransa ambao ndio wenyeji wa michuano ya Euro 2016, walianza kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Romania, Ufaransa wakiwa kwao walionekana kucheza kwa kujiamini na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, huku hali ya umiliki wa mchezo wakiwa wamemiliki mpira kwa asilimia 51 na Romania 41.


Magoli ya Ufaransa yalifungwa na Oliver Giroud dakika ya 57, goli ambalo lilidumu kwa dakika 8 tu na dakika ya 65 Romania wakasawazisha kwa mkwaju wa penati iliyopatikana baada ya Patrice Evra kucheza faulo na Bogdan Stancu kuitumia nafasi hiyo, furaha yaUfaransa ilirejeshwa na shuti la Dimitri Payet dakika ya 89 baada ya kuingia wavuni.
Video ya magoli ya mechi ya France 2 – 1 Romania


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments