May 27, 2016

Vanessa na Shilole kumaliza ‘bifu’ yao Billz, ilipangwa au mtu kachukua fursa?

Katika badiliko kubwa la matukio, Vanessa Mdee na Shilole wanatarajia kutumbuiza pamoja Jumapili hii kwenye ukumbi wa Club Billcanas jijini... thumbnail 1 summary
Katika badiliko kubwa la matukio, Vanessa Mdee na Shilole wanatarajia kutumbuiza pamoja Jumapili hii kwenye ukumbi wa Club Billcanas jijini Dar es Salaam.


Tangazo hilo limepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa muziki hasa ukizingatia kuwa ni juzi tu wawili hao walikuwa wakirushiana vijembe mtandaoni.

Shishi alienda mbali zaidi kwa kumtishia Vee kumchapa vibao wakikutana. Kwa wengi, nikiwemo mimi tuliamini kuwa madiva hao walikuwa wamemaindiana kweli. Video zao zilikuwa real!

Na sasa baada ya kuona hii show ya Billz kuna maswali mawili ya msingi kujiuliza. Kwanza, drama hiyo ilitengenezwa kama kiki ya show hiyo? Majibu yanaweza kukinzana na obvious wao wenyewe ndio wanajua ukweli ni upi. Chochote kinaweza kutokea kwenye showbiz.

Pili, Vee na Shishi walizinguana kweli lakini kuna mjasiriaburudani mmoja ameona fursa kwa kuwaambia ‘Vee kamata huu mpunga wako, Shishi chukua huu pandeni stejini tupige hela.’ Hiyo ndio showbiz my friends!

Kitu kimoja ambacho Vanessa na Shilole inabidi wakivumilie ni matusi kwa kwenye Instagram kutoka kwa mashabiki wanaoamini waliingizwa mkenge na vijembe vyao.

Vanessa ameandika; Talk is cheap. Tukutane Bilicanas. Umeongea sana. Tukutane jukwani Jumapili huku Shilole akijibu: Veee are u sure????:oops::oops:….

Yetu macho.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments