May 13, 2016

MAKONDA AMKINGIA KIFUA RAIS MAGUFULI

Mwaka jana zilisikika kila mahali sauti za baadhi ya Watanzania kwamba “TANZANIA INAHITAJI RAIS DIKTETA” kulingana na kile walichodai walic... thumbnail 1 summary
Mwaka jana zilisikika kila mahali sauti za baadhi ya Watanzania kwamba “TANZANIA INAHITAJI RAIS DIKTETA” kulingana na kile walichodai walichoshwa na hali ya nchi.
Baada ya Rais Magufuli kuuvaa uhusika kwa ajili ya Watanzania hao sasa hali imekuwa tofauti na anaanza kuitwa Dikteta jambo linalomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutamka kuwa ‘RAIS MAGUFULI SIO DIKTETA’.

Katika mahojiano yake na Kipindi cha Clouds360 cha Televisheni ya Clouds Makonda amesema wote wanaolalamika kuhusu utendaji wa Rais Magufuli wanakosea na hivyo wanatakiwa kukumbuka kuwa Rais huyo ni zao la marais wa awamu ya 3 na 4.
“Wale wanaolalamika Rais ni dikteta wanakosea na wakumbuke Rais ni zao la awamu ya 3 na ya 4 na katika awamu mbili miaka 20 kuna vitu ambavyo alijifunza na kimoja wapo alibaini ukitoa majukumu bila msukumo wengi hawafanyi”.

Makonda amesisitiza kuwa serikali ya awamu hii haitamvumilia mtumishi yeyote wa Umma ambaye hatokuwa karibu na wananchi wake anaowahudumia ambapo amewatolea mfano baadhi ya watumishi kwenye mkoa wake.
“Hakuna mtu anayemtambua Afisa Utamaduni na kimsingi ni mtu ambaye anatakiwa kuwa na ukaribu na wasanii katika kazi zao, Afisa Biashara wangu nenda kamuulize kama anajua kuna watu wangapi walitaka kufanya biashara wakashindwa, wao wanachokijua ni kutoa leseni na kuwapigia simu wafanyabiashara kufunga biashara zao au kuwapa pesa”.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments