March 09, 2015

HABARI KUBWA LEO,RAIS KIKWETE KUUMBUKA,NI KURA YA MAONI,DOKTA SLAA ASEMA ANAOTA NDOTO ZA MCHANA SOMA HAPA KUJUA

UWEZEKANO wa Watanzania kupiga kura ya Maoni ya Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba kama inavyong’ang’aniwa na Rais J... thumbnail 1 summary



UWEZEKANO wa Watanzania kupiga kura ya Maoni ya Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba kama inavyong’ang’aniwa na Rais Jakaya kikwete na Chama cha Mapinduzi CCM kwamba Kura hiyo ipigwe Tarehe 30 April mwaka huu,sasa umeota Mbawa,Anaandika KAROLI VINSENTEndelea nayo
Kukwama huku kwa kura ya maoni kunatokana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC,kushindwa katika uandikishaji wapiga kura unaofanyika kwa mfumo wa Biometric Voters Regislation,(BVR) kutokana na ukosefu wa Vifaa pamoja na kupewa mda mdogo.


Kwa Mujibu wa Mtoa Taarifa wetu kutoka Kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC ameumbia Mtandao huu kwa sasa wako mbioni kusitisha zoezi la kura ya Maoni ya kuamua Katiba pendekezwa.
“Sikufichi hapa tunafosiwa na Rais tufanye tuwezavyo tuwe tumemaliza Mwezi wa nne wakati uwezekano ni mdogo,kwasababu Daftari la kudumu haliwezi kukamilika kwa mda huo.yaani kama vifaa vikiwepo vyote vinavyoitajika basi Daftari linaweza kukamilika mwishoni mwa mwezi juni,yaani hapa hata wafanyaje hiyo kura haipigiki mwezi wanne”ameeleza.
Kuibuka kwa taarifa hizi kunakuja siku chache baada ya vyanzo vyetu kuambia mtandao huu kwamba Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi ccm,CC kilichoketi mwishoni mwa wiki iliyopita kilichofanyika chini ya Rais Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam kimekiri kwamba kura ya maoni kwa sasa haitoweza kufanyika kama ilivyopangwa.
Baadala yake Chama hicho kwa kumtumia Rais Jakaya Kikwete kitangaza mda wowete kutoka sasa Siku tofauti ya Kupiga kura ya Katiba hiyo iliyopendekezwa ambayo inatokana na Katiba iliyojaa utata wa Hali ya juu katika kupitishwa kwake ndani ya Bunge.
Taarifa za Kumanika ambazo mtandao huu umedokezwa zinazidi sema hadi kufikia jana,NEC ilikuwa na mashine 250 tu za kuendesha zoezi hilo,huku matatizo mengi yakiwa yamejitokeza katika uandikishaji wake unaoendelea Mji mdogo wa Makambako Mkoani Njombe.
Mtoa taarifa huyo alizidi kuambia mtandao huu kwamba Shehena ya Mwisho ya Vifaa inatarajiwa kuwasili nchini katikaki ya mwezi Juni mwaka huu.
Kwa mujibu la Andishi laNEC lilisema tume hiyo inahitaji mashine 15,000,Lakini serikali imeridhia kununuliwa mashine 8000,jambo la kushangaza NEC imepewa Mashine 250 tu kuendesha zoezi hilo ,Mradi huo ambao unagharimu zaidi ya Bilioni 293 za kitanzania.
Kulazimishwa huko na Rais Kikwete kwa tume ya uchaguzi ili kuharakisha uandikishaji wa wapiga kura kunakuja huku ikiwa tayari vyama vikuu vya Upinzani nchini kupitia umoja wao kutaka kura hiyo ya Maoni isitishwe kwa kuwa haitoweza kufanyika kwa ufanisi na kwamba badala yake serikali iwekeze nguvu zake katika kufanikisha uchaguzi mkuu utakofanyika baadae mwa mwaka huu.
Mbali na Vifaa vya uandikishaji huo,umekuwa na mapungufu mengi yamejitokeza ambao watendaji wa NEC wamethibitisha kutokea.
“Waandikishaji wanababaika,watu wengi,wanapanga foleni kutwa zima,halafu mara waambiwa kamera,halafu mara wanaambiwa mashine mbovu tena wanaambiwa kamera imegoma”
“La ajabu zaidi tumeshuhudia mashine imeshindwa kusoma alama za vidole wenye usugu” ameeleza mtoa taarifa wetu wa NEC aliyoko Makambako
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa ameuoambia Mtandao huu kwamba kwa sasa ni wazi Rais Jakaya kikwete anaota ndoto ya za Mchana mchana kuhusu upigaji kura wa Katiba iliyopendezwa na Bunge, kwani hata wanaomzunguka wanamdanganya.
‘Kura maoni hawezi kufanyika katika mda huu wanaosema wao,kwasasabu mpaka sahivi tume hiyo ipo Kwenye kata tatu tu huko Makambako tu na wametumia wiki zaidi nne,je hebu kata za nchi nzima watatumia mda gani, ambazo zipo zaidi ya mia nne ?tunavyosema kwamba kunaubabaishaji ndio huu”amesema Dokta Slaa.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: