Kelly Rowland na mtoto wake… Bado anamficha sura yake, hapa wako zao studio
Imekuwa tabia ya wasichana wengi na wanawake wanapopata watoto muda mfupi tu utaona wanaweka picha za watoto wao kwenye mitandao ya kijam... 10:16
Imekuwa tabia ya wasichana wengi na wanawake wanapopata watoto muda mfupi tu utaona wanaweka picha za watoto wao kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram, kwaKelly Rowland haijawa hivyo.
Picha ambazo tumebahatika kuziona za mtoto wa Kelly ni zile alizowahi kuweka, moja ya kichwa cha mtoto wake, ya pili ya mkono.
Moja ya vitu ambavyo mapaparazzi wanamuwinda ni kupata picha inayoonyesha sura ya mtoto huyo hasa akiwa naye mtaani, bado hawajapata mpaka sasa.
Picha aliyoshare mara ya mwisho kwenye ukurasa wake wa Instagram inamuonyesha akiwa amekaa studio na mtoto wake wa kiume Titan, amemlaza kifuani kwake na kumfunika vizuri bila kuandika chochote.