December 16, 2014

Wakati uhusiano wa mastaa wengi ukiyumba, hawa wamedumu kwa zaidi ya miaka 15…

Ni December ambayo tunashuhudia rekodi mbalimbali zikiingia kwenye kumbukumbu za mwaka huu, tumesikia sana ya Chris Brown na Karrueche, J... thumbnail 1 summary
david-victoria-beckhamNi December ambayo tunashuhudia rekodi mbalimbali zikiingia kwenye kumbukumbu za mwaka huu, tumesikia sana ya Chris Brown na Karrueche, Justin Bieber na
Selena Gomez, Nick Minaj na wengineo ambao huu mwaka haukuwa na heri kwenye ulimwengu wa uhusiano wa kimapenzi.
Kumekuwa na story za mastaa wengi vijana ambao uhusiano wao unayumba kila siku, kumbe wakati wengine wakiyumba wapo ambao wanasherekea ndoa zao kudumu muda mrefu.
Mastaa wawili David Beckham na mke wake Victoria wameoana tangu mwaka 1999, sherehe ya ndoa yao ni moja ya sherehe zilizohudhuliwa na watu wachache zaidi ambapo wageni waalikwa walikuwa 29 tu.
Mpaka sasa mastaa hao wana watoto wanne, mbali ya maisha yao kuwa ya kuhama hama lakini bado ndoa yao ni moja kati ya ndoa za mastaa vijana ambazo zimedumu muda mrefu zaidi na bado zinaonekana imara.
David-Beckham-With-Family
David Beckam na Victoria wakiwa matembezi na familia yao.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: