August 13, 2014

WEMA SEPETU; NAJUTA SANA KURUDIANA NA DIAMOND

Takribani wiki sasa kumekuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu hayuko sawa katika mahusiano yake ya kimapenzi... thumbnail 1 summary

Takribani wiki sasa kumekuwa na
taarifa zinazoeleza kuwa Miss Tanzania
2006, Wema Sepetu hayuko sawa
katika mahusiano yake ya kimapenzi
na nguli wa Bongo Fleva, Diamond
Plutnumz….

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu na
Wema, imefika mahali Wema anajuta
kuwa na Diamond kwa sababu ya
kuandikwa kwa mambo mengi yasiyo
na ukweli na yanayomfedhehesha
moyoni….
Rafiki huyo amedai kuwa mara kwa
mara Wema amekuwa akijiuliza
sababu ya kuandikwa taarifa
mbalimbali zisizo na kichwa wala
miguu ambapo mwisho wa yote
hupata jibu ni kwa sababu ya kuwa
na mahusiano na Diamond….
“Wakati mwingine anasema angelijua
bora angebaki bachela kwani kuna
kikundi cha watu hakipendi kumuona
akiwa na Diamond hivyo kinafanya kazi
ya kumzushia taarifa zisizoeleweka kila
mara kwa lengo la kumshushia hadhi,”
kimesema chanzo hicho.
Mwandishi alipokiuliza chanzo hicho
ni kwa kiasi gani Wema anamwamini
Diamond kilisema:

“Ukweli ni kwamba Wema anampenda
sana Diamond lakini hamwamini kwa
sababu wakati mwingine taarifa
zinazoandikwa magazeti hutolewa na
Diamond mwenyewe, hali hiyo inampa
wakati mgumu sana Wema kujua ashike
wapi na wapi apaache, “Unajua Diamond haaminiki, unaweza
kukuta Wema anagombana na watu
kumbe mtoa taarifa ni Diamond
mwenyewe.”


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: