June 26, 2014

Uchaguzi Mkuu CUF: Profesa Lipumba na Maalim Seif WAPETA katika nafasi zao za Mwenyekiti Taifa na Katibu mkuu

Mkutano Mkuu wa CUF Taifa umemchagua tena Katibu Mkuu wa Chama hicho kuendelea na wadhifa huo kwa kupata kura 675, sawa na asilimia ... thumbnail 1 summary

Mkutano Mkuu wa CUF Taifa umemchagua
tena Katibu Mkuu wa Chama hicho
kuendelea na wadhifa huo kwa kupata
kura 675, sawa na asilimia 99.5 ya kura
zilizopigwa.
Mkutano huo pia umemchagua Prof.
Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF
Taifa kwa kupata kura 659 sawa na asilimia
95.5 na kumshinda mpinzani wake Chifu
Lutalosa Yemba aliyepata kura 30 sawa na
asilimia 4 nukta 3.

Aidha mkutano huo umemchagua Mhe.
Juma Duni Haji kuwa Makamu Mwenyekiti
wa Chama hicho kwa kupata kura 662
sawa na asilimia 99.25.
Akizungumza baada ya kutangazwa
mshindi Katibu Mkuu wa Chama hicho
Maalim Seif Sharif Hamad, amewapongeza
wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumpa
tena ridhaa ya kuongoza chama hicho kwa
kipindi cha miaka mitano ijayo.
Wakati wa Kampeni. Mapema akizungumza
katika kampeni za kuomba kuchaguliwa
tena kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho,
Maalim Seif amesema siri ya mafanikio yake
kisiasa ni kutokana na kujiamini kwake
kuwa kiongozi, kuwa mkweli na kuwa na
dhamira
njema kwa wananchi.
Akijibu hoja za wajumbe wa mkutano huo
Maalim Seif amewataka viongozi wa chama
hicho kutotangaza kuhudhuria kwa
viongozi wa kitaifa kwenye mikutano ya
hadhara hadi pale wenyewe
watakapothibitisha kuhudhuria, ili
kuepusha wananchi kutoamini utendaji wa
viongozi hao.
Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti
wa Chama hicho Mhe. Juma Duni Haji
wakati wa kampeni alisema iwapo
atachaguliwa kushika nafasi hiyo
atashirikiana na viongozi wengine wa
kitaifa pamoja na wananchi kuhakikisha
kuwa chama kinapata maendeleo zaidi.
Chifu Yemba alisema ameamua kugombea
nafasi hiyo kutetea demokrasia ya kweli
ndani ya chama na taifa kwa ujumla. Chifu
Yemba ambaye ni mwanasayansi kitaaluma,
pia ni Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya
Shinyanga Mjini.
Prof. Lipumba wakati wa kampeni alisema
akichaguliwa atahakikisha anatembelea
nchi nzima kuimarisha chama kabla ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Aidha
amesema atafanya juhudi za ziada kuona
kuwa Tanzania inakuwa na
Muungano wa
kuheshimiana baina ya pande mbili za
Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar).
Amesema wanawake watapewa nafasi
ndani ya kamati tendaji ya chama
kuondosha dhana ya mfumo dume
unaodaiwa kuwepo katika ngazi za juu za
uongozi.
Mgombea mwingine wa nasafi ya
Mwenyekiti wa CUF Taifa M'bezi Adam
Bakar, alijitoa kwenye kinyang'anyiro hicho
na kubakia wagombea wawili wa nafasi ya
Mwenyekiti.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF)
Ismail Jussa Ladhu aliteuliwa kuwa
mwenyekiti wa muda wa kuongoza
uchaguzi huo uliosimamiwa na
mwanasheria Awadh Ali Said

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: