June 26, 2014

Team Wema, Team Kajala Kuvunjwa.....Yadaiwa ndo chanzo cha Ugomvi wa Wema Sepetu na Kajala.

Makundi mawili hasim ya wasanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja yajulikanayo kama 'Wema Team' na 'Kajala ... thumbnail 1 summary

Makundi mawili hasim ya wasanii wa
filamu Bongo, Wema Sepetu na Kajala
Masanja yajulikanayo kama 'Wema Team'
na 'Kajala Team' yanatarajiwa kuvunjwa
kwani ndio yameonekana kuchochea
bifu la wawili hao ambalo limekuwa
likionekana kuisha na kuibuka tena....
Akizungumza na mwanahabari wetu,
Kajala amesema kuwa tatizo lao

limekuwa likichochewa na makundi
hayo hasa wanapotangaza kusamaheana
na kuzika tofauti zao makundi hayo
huibuka na kuanza kutukanana, kitu
ambacho huzusha tena hasira zao....
"Siyo siri, tatizo letu linachangiwa na hizi
team ambazo zipo kwa ajili ya
kuongeza matatizo.
Tunafikiria kuyavunja
kwani kwa sasa yameonekana
kutokuwa na faida zaidi ya kuzidisha
hasira ambazo tumekuwa tukizizika kila
tunapotangaza kusameheana," alisema
Kajala.
Msanii huyo alisema hawaoni haja ya
kuwa na makundi ambayo hayawatakii
mema kwani katika maisha kukosana
kupo lakini pia kusameheana ndo
jambo la busara kwani hakuna
aliyemkamilifu hapa duniani.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: