May 23, 2014

MAKUBWA MCHUMBA WA MAREHEMU KUAMBIANA AIBUKA

MAMBO  yameanza! Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuk... thumbnail 1 summary
MAMBO yameanza! Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka na
kusema alikuwa mchumba wa marehemu, Ijumaa linakujuza.
Mrembo anayejulikana kwa jina la Lulu Jumanne ‘Selina’.
Kwa mujibu wa mrembo huyo, Lulu Jumanne ‘Selina’, alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa yake haipo sawasawa.
Alisema walianzisha uhusiano lakini haukuwa wazi katika jamii. Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala, wazazi wake walimtembelea.
“Nikiwa na wazazi nilimwona Kuambiana anapiga hodi, akaingia akiwa na  begi la nguo. Niliogopa kwani
wazazi walikuwepo na walikuwa hawamtambui.
Lulu Jumanne ‘Selina’, akiwa na marehemu Kuambiana.
“Hata hivyo, walielewa yakapita, tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua,” alisema Selina ambaye naye ni mwigizaji.
Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya hapo maisha yaliendelea lakini ikafika mahali marehemu akahamishia mapenzi kwa Mbongo Fleva, Stara Thomas yeye akawa ‘zilipendwa’.
Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao.
Katika mahojiano mafupi kati ya Selina na gazeti hili, mambo yalikuwa hivi:
Ijumaa: Mlikuwa na mipango gani ya maisha?
Selina: Mingi tu. Kwanza alishanitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake na wadogo zake.
Ijumaa: Marehemu alionesha upendo wa dhati kwako?
Selina: Sana tu, kwani alipenda kuniita mke wake. Alikuwa ananiheshimu hadi mwisho. Hakuwa akipenda
mwanaume anizoee.
Ijumaa: Unajua nini kuhusu kuumwa kwake?
Selina: Najua alikuwa anaumwa tumbo kwa muda mrefu. Alikuwa akila chakula cha maelekezo ya daktari.
Ijumaa: Mara ya mwisho ulizungumza naye nini?
Selina: Nilimshauri anunue simu yenye WhatsApp kwani mara nyingi Kuambiana alikuwa hapatikani hewani. Alikuwa hawezi kukaa na simu kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Selina alisema hapendi kueleza mengi lakini anaamini yeye ndiye mwanamke wa mwisho katika mapenzi na marehemu.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: