May 14, 2014

Loveness Diva kufanya Video ya ‘Mashallah’ na Director wa Kenya

Diva The Bawse ambaye ametoa wimbo wake mpya  ‘Mashallah’  siku chache zilizopita, amesema anajiandaa kuufanyia video pamoja na kuanza ... thumbnail 1 summary

Diva The Bawse ambaye ametoa wimbo wake mpya ‘Mashallah’ siku chache zilizopita, amesema anajiandaa kuufanyia video pamoja na kuanza tour ya kuutangaza wimbo huo.


“Video tunatarajia kufanya na aliyefanya ‘Asante’ ya Ay,” Diva ameiambia Mpekuzi leo.
Ameongeza kuwa kwasasa ameamua kuingia kwenye muziki kwa miguu yote miwili, ndio sababu anatarajia kuanza kufanya tour mikoani kuutangaza wimbo wake.
“Nahitaji kutumia muda mwingi kuutangaza huu wimbo, ambao uko chini ya management ya Sharobaro Recs, na ningependa kuulizwa maswali yanayohusu muziki zaidi kuliko mambo binafsi, nahitaji kuwa na privacy na ku-focus na biashara yangu, maisha yangu ya radio na muziki.”Alisema Diva  na  kuongeza

 
“Pia nina meneja mpya anaitwa Kerry Kerwin ambaye anamsimamia Victoria Kimani akiwa hapa Tanzania, na pia niko tayari kuanza kufanya shows za mikoani. Tutahakikisha huu wimbo unafika katika radio zote za mikoani Tanzania na nje, na habari njema ni kuwa ‘Mashallah’ imeanza kupigwa Nairobi.”

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: