May 14, 2014

DIAMOND PLATNUMZ ATUA UINGEREZA KUSHOOT VIDEO MPYA, AONGOZANA NA OMMY DIMPOZ! PICHA ZIPO HAPA

Mshindi wa tuzo saba za KTMA 2014 Nasib Abdul aka Diamond Platnumz aka ‘Chibu’ na Ommy Dimpoz wameondoka Tanzania thumbnail 1 summary


Mshindi wa tuzo saba za KTMA 2014 Nasib Abdul aka Diamond Platnumz aka ‘Chibu’ na Ommy Dimpoz wameondoka Tanzania
jana kuelekea nchini
Uingereza.
Platnumz na Dimpoz wakati wa safari yao ya UK jana
Diamond ameshare baadhi ya picha za safari hiyo akiwa ameongozana na Ommy Dimpoz pamoja na meneja wake Babu Tale.
Licha ya kuwa Platnumz hajasema kilichompelela Uingereza, lakini mpenzi wake Wema Sepetu kupitia ‘You Heard’ ya XXL, amethibitisha kuwa ‘baby’ wake pamoja na mambo mengine pia ameenda kushoot video.

Asante mungu tumefika salama in London, ameandika Tale
Hivi karibuni hit maker wa ‘Number 1′ alipokuwa Nigeria alisema ataenda Uingereza kushoot video ya wimbo wake mpya unaotarajiwa kutoka mara baada ya kukamilika.


Jumamosi iliyopita Platnumz aliwaomba radhi mashabiki wake wa Uingereza kwa kushindwa kufika kwaajili ya show iliyokuwa imepangwa kufanyika siku hiyo (May 10) na kuahidi kuwa angesafiri siku si nyingi kwenda London kwaajili ya show hiyo.
Chanzo: Bongo5.com

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: