May 10, 2014

ELIMU KWA KIJANA:KUTO KUKATA TAMAA NI ISHARA YA MAFANIKIO

Kuanza safari sio ishara ya kumaliza,kua na ndoto sio ishara kwamba itatimia na pia kua na shahada nzuri katika masomo sio ishara kwamba... thumbnail 1 summary
Kuanza safari sio ishara ya kumaliza,kua na ndoto sio ishara kwamba itatimia na pia kua na shahada nzuri katika masomo sio ishara kwamba
Umeshinda maisha hivyo ni vizuri kutambua umuhimu wa kuto kukata tamaa katika maisha kwasababu hiyo tu ndio ishara inayoleta tofauti kati ya mwenye hatima na mwenye safari fupi.
Ni muhimu kutambua kwamba unapokua na kitu kizuri basi lazima
Kutakutana na changamoto kwasababu tunaishi katika ulimwengu ambao utakushusha kila unapotaka kupanda ngazi ya mafanikio.
Changamoto ni moja ya dalili kwamba una kitu kizuri mbele yako na
Kama wewe una ndoto ambayo haina changamoto basi jua haitadumu
Kwasababu uimara wa ndoto yako ni ushindi unaopata katika kuzikabili
Changamoto zako. Ni muhimu kutambua kwamba changamoto ni
Kitu cha kawaida katika maisha ya mwanadamu na kama wewe hupendi
Changamoto basi hupendi kufanikiwa. Hakuna kitu kinachokua imala bila kupitia katika mazingira magumu. Mtazamo wako kuhusu changamoto ndiyo utakao kufanya ushinde ama zikushinde hizi changamoto.wenye mtazamo wa mafanikio wanaona changamoto kama dalaja la mafanikio na wasio na mtazamo mzuri wanaona changamoto kama kizuizi cha mafanikio na ukishakua na mtazamo kama huo basi utakua ni mtu wa kukwazika kila mara unapopitia Hali isiyo ya kawaida.   kwa mawasiliano au kujua zaidi.....



Facebook page: Elly David Tanzania


Tel:0688 440029

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: