March 30, 2014

CHAMELEONE ANYANG'ANYWA GARI AINA YA ESCALADE KWA KUSHINDWA KULIPA KODI

Jose Chameleone amenyang’anywa gari yake aina ya Escalade na maofisa wa URA baada ya mamlaka hiyo kudai kwamba msanii thumbnail 1 summary

Jose Chameleone amenyang’anywa gari yake aina ya Escalade na maofisa wa URA baada ya mamlaka hiyo kudai kwamba msanii
huyo ameshindwa kulipa kodi yenye thamani ya shilingi milioni saba ya Uganda.
Muda mchache kabla ya kuanza kwa onyesho kubwa la Tubonge la msanii huyo, maofisa wa URA waliikamata gari yake hiyo ya kifahari.

Kwa mujibu wa mtandao wa Redpapper wa nchini Uganda,msanii huyo alijaribu kuwakatalia wasikuchukue gari lake akidai atakufa na mtu atakayeichukua lakini kauli hiyo haikufua dafu kwa mamlaka hiyo. “Hii ni gari yangu binafsi na nina haki yake, mtu yeyote akigusa Escalade yangu, nami tufe pamoja naye,” alidai Chameleone.

Hata hivyo Chameleone alidai kuwa hana tatizo lolote kulipa kodi lakini mamlaka hiyo haikutolea vigezo walivyotumia kupata jumla ya shilingi milioni 7 za Uganda ambazo ndizo pesa wanazomdai


KWA HABARI MOTOMOTO BONYEZA HAPA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK NA WHATSAPP

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: