January 12, 2014

"DIAMOND NI WA "HAPA HAPA" MIMI WA INTERNATIONAL"...!!! BABY MADAHA AFUNGUKA..SOMA ZAIDI HAPA

Baby Madaha amesema kamwe hawezi kucheza ligi moja na Diamond Platnumz. Akiongea na kipindi cha Hot Mix cha EAT... thumbnail 1 summary

Baby Madaha amesema kamwe hawezi kucheza ligi moja na Diamond Platnumz. Akiongea na kipindi cha Hot Mix cha EATV Ijumaa hii, muimbaji na muigizaji huyo wa ‘The Gal Bladder’ amesema Diamond ni msanii ‘wahapahapa’ huku yeye akifahamika kimataifa zaidi

Aliongeza kuwa pamoja na kufanya muziki, yeye pia ni muigizaji mzuri wa filamu wakati Diamond ni muimbaji peke yake na hivyo kamwe hawezi kuwa level moja na hitmaker huyo wa Roho Yangu.

Kwa muda sasa, mafahari hao wamekuwa wakirushiana madongo huku Baby akisema Diamond hajui kuimba kulinganisha na msanii kama Ali Kiba.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments