December 16, 2016

Suarez hatimaye amekubali kujitia kitanzi Barcelona

Mchezaji wa klabu ya Barcelona Luis Suarez hatimaye amekubali kusaini mkataba mpya na vigogo hao wa soka nchini Uhispania utakaoafikia th... thumbnail 1 summary
Mchezaji wa klabu ya Barcelona Luis Suarez hatimaye amekubali kusaini mkataba mpya na vigogo hao wa soka nchini Uhispania utakaoafikia thamani ya Euro milioni 167 ikijumuisha kipengele cha kumuuza kwa timu itakayomuhitaji.


Taarifa kutoka Barcelona zinasema kuwa mkataba huo utakaomfunga Suarez mwenye miaka 29 mpaka mwaka 2021 utasainiwa siku ya leo Ijumaa.

Alifunga magoli 40 kwenye ligi kuu soka nchini Uhispania msimu uliopita.

Mshambuliaji Lionel Messi raia wa Argentina mwenye miaka 29 ana mkataba na klabu ya Barcelona mpaka mwezi June 2018 lakini mazungumzo ya mkataba mpya tiyari yameanza.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments