December 24, 2016

Ibrahim Ajibu atimkia Misri kuanza maisha mpya ya soka

Mshambuliaji fundi wa klabu ya wenkundu wa Msimbazi Simba SC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, Ibrahim Ajibu, ameondoka klabuni ha... thumbnail 1 summary


Mshambuliaji fundi wa klabu ya wenkundu wa Msimbazi Simba SC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, Ibrahim Ajibu, ameondoka klabuni hapo na kutimkia nchini Msri kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo awali zilidai kuwa Ajibu ameondoka bila kutoa taarifa kwa uongozi wa klabu, lakini baadaye meneja wa timu hiyo Musa Hassan Mgosi amethibisha kuwa uongozi una taarifa na umetoa baraka kwa mchezaji huyo kwenda kutafuta nje ya Tanzania.

“Ajibu kaenda Misri kwajili ya majaribio na kapata ruksa ya viongozi kama ilivyo ada ya klabu ya Simba, Simba haimzuii mchezaji wake akipata timu ya nje” Amesema Mgosi.

Ingawa Mgosi amesita kutaja timu ambayo Ajibu anakwenda, lakini taarifa zinaeleza kuwa anakwenda katika timu ya Harass El Hadood.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments