December 09, 2016

HATIMAE AFANDE SELE AFUNGUKA KILICHOMFELISHA 20 PERCENT, CHEKI VIDEO HII HAPA

Huwezi kuacha kumzungumzia msanii 20 Percent kama utaitaja list ya wasanii ambao wamefanya makubwa na kuishangaza jamii katika historia y... thumbnail 1 summary
Huwezi kuacha kumzungumzia msanii 20 Percent kama utaitaja list ya wasanii ambao wamefanya makubwa na kuishangaza jamii katika historia ya muziki wa Bongo Fleva.

Ni kutokana na makubwa aliyoyafanya katika tuzo za muziki nchini Tanzania (Kili Music Awards) mwaka 2011 kwa kutwaa jumla ya tuzo 5 kwa mkupuo. Lakini Tuzo hizo zilikuwa kama mkosi kwa msanii 20 Percent kutokana na kushuka kimuziki baada tu ya kutwaa tuzo hizo.

Mengi yameongelewa mitaani lakini leo Lindiyetu.com imepiga story na rafiki wa karibu wa 20 Percent toka enzi hizo ambaye naye pia ni msanii mkongwe wa Hiphop Tanzania Afande Sele na ameweza kutupa mtazamo wake ambao anahisi ndio sababu ya mshkaji wake 20 Percent kufeli kumuziki.

“Inabidi tuwe wakweli katika hili, Twenty ni msanii mwenye kipaji sana, kiasi kwamba mimi mpaka leo kwenye Top10 yangu Twenty huwa namuweka namba 1. Ni mbunifu na pia anapenda anachokifanya. Kurudi kwa Man Water sidhani kama ndio itakuwa sababu ya Twenty kurudi kwenye game, kwasababu hata kabla hajaanza kufanya kazi na Man Water Twenty alishafanya kazi na kina Brighton na alifanya vizuri tu. Mkwamo wa twenty haujasababishwa na kipaji kupotea wala kutofanya kazi na Man Water. mi nahisi kilicho mvuruga Twenty ni kupoteza nidhamu.”

Yapo mengi sana ambayo ameyaongea Afande Sele na ninakupa nafasi ya kumsikiliza mwenyewe akizungumza. Play hii video hapa chini kumsikiliza.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments