October 13, 2016

KIM KARDASHIAN AISHTAKI TOVUTI HII KWA KUANDIKA TAARIFA ZA UONGO..

Staa wa TV show na Babymama wa Kanye West Kim Kardashian ameishitaki Website ya “Media TakeOut” pamoja na Bosi wa mtandao huo kwa kile al... thumbnail 1 summary
Staa wa TV show na Babymama wa Kanye West Kim Kardashian ameishitaki Website ya “Media TakeOut” pamoja na Bosi wa mtandao huo kwa kile alichokidai ni uchafuliwaji wa jina baada ya mtandao huo kuripoti kama Kim alidanganya tukio lake la kuvamiwa mjini Paris.
Kim Kardashian amesema baada ya kuwa “mwathirika wa tukio hilo la wizi wa kutumia silaha Ufaransa, Kim Kardashian alirejea Marekani na kujikuta tena anakuwa mwathirika kwa mara nyingine, wakati huu mwathiriwa wa gazeti la udaku lililochapisha habari kuhusu yeye kuwa ni muongo na hakuvamiwa kama anavyowadanganya watu.
Kwenye kesi hiyo, anataka alipwe kiasi cha pesa ambacho hakikutajwa mara moja.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments