October 14, 2016

Dully Sykes asema ana nyimbo 6 ndani ambazo amemshirikisha Diamond

Msanii wa muziki, Dully Sykes amesema mpaka sasa ana nyimbo sita ndani ambazo amemshirikisha Diamond Platnumz lakini hafikirii kuziachia. thumbnail 1 summary
Msanii wa muziki, Dully Sykes amesema mpaka sasa ana nyimbo sita ndani ambazo amemshirikisha Diamond Platnumz lakini hafikirii kuziachia.


Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Inde’ akiwa amemshirikisha ‘Harmonize’ wa WCB, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa kwa sasa atakuwa anakwenda na mwendo wa kutoa kolabo tu.

“Sipo WCB Wasafi na wala sijasaini wasafi ila nipo nao karibu na nafanya kazi nao karibu, mpaka sasa nimefanya kazi zaidi ya sita na Diamond Platnumz na sifikirii kama zitatoka saizi,” alisema Dully Skyes

Pia muimbaji huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki, amesema kwa sasa ameanza maandalizi ya kazi yake mpya ambayo pia amedai ni kolabo.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments